ALIYEWAHI
kuwa Katibu Mkuu wa Dar es salaam Young Africans George Johnson
Mpondela ‘Castor’ amefariki dunia jana saa nne usiku katika hospitali ya
Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya moyo.
Amesema msiba uko nyumbani kwao, eneo la Karakata, Uwanja wa Ndege karibu na Kanisa Katoliki na kituo kidogo cha Polisi, maarufu Polisi Posti.
Marehemu ameacha mke na watoto tisa, ambao ni Pius, Robert, Hilton,
Kennedy, Joseph, Collin, na wa kike Linda, Jaqcueline na Jennifer.
Hilton amesema mwili wa marehemu utasafirishwa Jumanne kwenda Tabora baada ya kuagwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hospitali ya Muhimbili tayari kwa mazishi yake Jumatano kijiji cha Misha wilaya ya Tabora vijijini.
MJUMBE Sr

Post a Comment