Unknown Unknown Author
Title: GODLISTEN MALISA:UHAMIAJI WAME KIUKA SERA ZA SHIRIKA LA KAZI DUNIANI! ....NI USAILI WA HOVYO PIA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
1.   KAULI   YA  BW   MALISA   GODLISTEN    KUPITIA    UKARASA  WAKE    WA   FACEBOOK   UKISTAAJABU YA UHAMIAJI UTAONA YA...

1.   KAULI   YA  BW   MALISA   GODLISTEN    KUPITIA    UKARASA  WAKE    WA   FACEBOOK
 
UKISTAAJABU YA UHAMIAJI UTAONA YA UTUMISHI..!!

Juzi (ijumaa) idara ya Uhamiaji ilifanya usaili kwa jumla ya vijana 10,846 ili kupata vijana 70 tu watakaoajiriwa kama Maafisa Uhamiaji wasaidizi. Hii ilikua ni wastani wa 1/156 yaani nafasi moja ya kazi ilishindaniwa na watu 156.

Uwezekano wa kupata nafasi kwa vijana waliojitokeza kufanya usaili (probability) ilikua 0.0064.

Kwa lugha nyingine ni ...kwamba kila kijana aliyejitokeza kwenye usaili ule uwezekano wa kupata kazi ni asilimia 0.64% na uwezekano wa kukosa ni asilimia 99.36%.

Kwa maneno mengine ni kuwa uwezekano wa kupata kazi ni chini ya asilimia moja (possibility is less than 1%). Rekodi hii ni ya kwanza kutokea duniani.

Kabla ya rekodi hii, nchi iliyokua ikishikilia rekodi ni China. Mwaka jana kiwanda kikubwa zaidi cha nguo duniani kiitwacho China Textile Industry, kilichopo mjini Keqiao, kwenye Kaunti ya Shaoxing jijini Shanghai, kilifanya usaili kwa watu zaidi ya laki moja wakitafuta kuajiri watu 5,000 tu.

[Kiwanda hiki kina wafanyakazi zaidi ya elfu hamsini na vibarua zaidi ya laki 2 wanaofanya kazi kiwandani hapo kila siku].

Kufanya usaili kwa watu laki moja ili kupata waajiriwa 5,000 inamaanisha uwezekano wa kupata kazi kwa kila mtahiniwa (probability) ilikua 0.05.

Kwa lugha nyingine ni kuwa uwezekano wa kupata kazi kwa watahiniwa ulikuwa 5% na uwezekano wa kukosa ulikua 95%.

Jumuiya ya kimataifa ililaani kitendo hiki na usaili huu ukaingia kwenye rekodi za dunia kuwa ni usaili wa hovyo zaidi kuwahi kutokea duniani. (The world most ridiculous job interview ever happened).

Taarifa zinasema kuwa haikua haki (it was unfair) kumdahili mtu huku uwezekano wa kupata kazi hiyo ukiwa chini ya asilimia 5%. Ilionekana ni uonevu.

Vyanzo vya habari vilivyopinga usaili huo vinasema, Shirika la kazi duniani (ILO) linapendekeza usaili wa kazi uwape uhakika wa zaidi ya 50% wanaosailiwa.

Hii ina maana kuwa mtu anayefanyiwa usaili wa kazi anapaswa kuwa na uhakika wa angalau 50% wa kupata kazi wakati anapofanyiwa usaili.

Asilimia 50% maana yake ni kuwa idadi ya wasailiwa isizidi mara mbili ya nafasi za kazi zilizopo. Kwa mfano kama nafasi ni 70 unapaswa kufanya usaili kwa watu wasiozidi 140.

Katika nafasi 70, ukisaili watu 140 maana yake ni kwamba kila aliyeitwa kwenye usaili ana uhakika wa kupata kazi wa 50%. Hivi ndivyo ILO wanavyopendekeza. Yani uhakika uwe 50% au zaidi.

Na hivi ndivyo mashirika mengi ya kimataifa yanavyofanya. Kama nafasi ni 3 hata mkiomba 100 uwezekano wa kuitwa kwenye usaili (interview) ni watu 6 tu' ili katika hao 6 wapatikane watatu watakaoajiriwa (sawa na 50% ya waliodahiliwa).

Sasa Idara ya Uhamiaji wakaamua kwa makusudi kuvunja rekodi ya China na kuiweka Tanzania kwenye kilele. Wakati China ikipigiwa kelele kwa kuweka uwiano wa asilimia 5%, Uhamiaji wao wakaenda mbali zaidi kwa kuweka uwiano wa asilimia 0.64%

Hali hii iliwafanya Watanzania wengi kulaani mfumo huu wa usaili uliotumiwa na idara ya UHAMIAJI kwa sababu kuu mbili.

Kwanza ni mfumo wa udhalilishaji. Huwezi kuwakusanya wasomi kwenye uwanja wa mpira kama magunia ya vitunguu ili wafanye usaili wa kazi. Aina hii ya usaili ilikiuka misingi ya utu (it was agaist human dignity).

Pili usaili huu ulizidi kudhoofisha hali ngumu za kiuchumi walizonazo vijana hawa. Gharama za nauli (kwa waliotoka mikoani), malazi na chakula walizotumia ni wizi wa kusadikika uliofanywa na serikali (ya CCM).

Ikiwa kila kijana alitumia wastani wa 150,000/= kama gharama za nauli, malazi na chakula kwa siku alizokaa Dar, ukizidisha kwa watu 10,000 utapata jumla ya shilingi Billion Moja na milioni mia tano (1.5 billlios).

Fedha hizi ni nyingi kuliko fedha zote za miradi ya maendeleo kwenye wizara ya Afrika Mashariki. Ni nyingi kuliko madai ya askari Magereza wote nchini. Askari magereza wanadai jumla ya bilioni 1.2 ikiwa ni malimbikizo ya posho zao mbalimbali, ghamama za uhamisho n.k.

Hebu fikiria vijana wasio na kazi wala chanzo chochote cha mapato unawapora Bilioni moja na milioni mia tano, kwa kisingizio cha kuwaita kwenye usaili.!!!

Tena usaili wenyewe uwezekano wa kupata kazi ni chini ya asilimia moja (1%).!!! Huu mi uhuni na ukatili usioweza kuvumilika. Mbaya zaidi ukatili huu umefanywa kwa makusudi na serikali (ya CCM).

Lakini wakati hayo yote yakiendelea kuna kioja kingine kikubwa kimetokea. Lakini hakijasikika sana labda kwa kuwa kila mtu alikua "busy" na kioja cha idara ya UHAMIAJI.

Kioja chenyewe ni hiki. Menejimenti ya utumishi wa umma ilitangaza nafasi za kazi. Vijana zaidi ya 4,000 wakaomba nafasi mbalimbali zilizotangazwa.

Wote wakaitwa kwenye usaili. Usaili wenyewe ulikua jana (jumamosi) pale chuo cha Mwl.Nyerere Kigamboni.

Hakuna aliyedhani kama UTUMISHI wangeweza kurudia makosa ya UHAMIAJI. Lakini kilichotokea ni kinyume chake. Idadi ya watu haikua kubwa sana kama ile ya Uhamiaji lakini nafasi zilikua chache zaidi ya zile za Uhamiaji.

Kwa mfano nafasi ya maafisa maendeleo ya Jamii (Community Dev.Officers) iliombwa na watu 716, walioshiriki usaili jana ni watu 564. Lakini nafasi za kazi (vacancy) kwa maafisa maendeleo ya jamii zilikua mbili tu.

Hii inamaanisha kuwa vijana wote 564 waliofanya usaili jana kwenye nafasi ya maafisa maendeleo ya jamii, walikua wanapigania nafasi mbili tu za ajira.

Huu ni uwiano wa 0.35% au 1/282. Yani kati ya watu 282 waliofanya usaili ataajiriwa mmoja, halafu mwingine mmoja atapatikana kati ya 282 waliosalia.

Hii ni sawa na kusema vijana wote walioshiriki usaili huu kwenye nafasi tajwa hapo juu wana uhakika wa kupata ajira kwa 0.35% na uhakika wa kukosa ni 99.65%.

Hiki ni kiwango cha juu zaidi ukilinganisha na kile cha UHAMIJAJI ambako uhakika wa kupata ajira ulikua angalau 0.64% na kukosa 99.36%.

Hii inamaanisha kuwa UTUMISHI wamevunja rekodi ya dunia iliyowekwa na idara Uhamiaji. Kwa lugha rahisi ni kuwa Uhamiaji walishikilia rekodi kwa siku moja tu kisha Utumishi wakaivunja.

Hivyo basi napenda kuchukua fursa hii kutangaza kuwa Menejimenti ya UTUMISHI WA UMMA nchini Tanzania kwa sasa ndiyo inayoshikilia rekodi ya dunia ya kufanya usaili wa kazi wa hovyo kuliko usaili mwingine wowote uliopata kutokea duniani (The world most ridiculous job interview).

Hongera idara ya Utumushi kwa kupata nafasi hiyo. Pongezi kwa mama Hawa Ghasia na serikali nzima (ya CCM) kwa kutekeleza vema Ilani ya chama chenu. Ama kweli ukistaajabu ya UHAMIAJI utayaona ya UTUMISHI.

***JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.
Alamsiki.. || Malisa GJ.!


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top