Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Ernest Mangu |
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limewafukuza kazi
askari polisi wake wanne wakiwemo watatu wa kikosi cha usalama barabarani ambao
wamefukuzwa kwa kosa la kupokea rushwa na kwenye magari barabarani na askari mwingine
kwa kosa la utoro jeshini baada ya kujipa likizo mwenyewe.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi mkoa
wa Shinyanga kwa vyombo vya habari iliyotolewa Juni 16 ,2014 na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
kamishina msaidizi wa polisi Kihenya Kihenya.
Kamanda Kihenya amesema kwa mujibu wa mamlaka aliyokasimiwa
na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IJP amewafukuza
kazi askari polisi hao kwa fedheha kuanzia Juni 11,2014 kwa kosa la kufanya
kitendo kibaya kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la polisi cha kupokea rushwa
wakiwa kazini tarehe 30,Machi,2014 majira ya mchana.
Kamanda Kihenya amewataja askari wa kikosi cha usalama
barabarani waliofukuzwa kazi kuwa ni EX.F.899 koplo Jonathan James Bujiku,EX.WP.5198
Pc Joyce Malima Paul na EX.F 9839 pc Sohela Mabeho Kisinza.
Amesema askari hao walipokea rushwa ambayo thamani yake
haikufahamika kutoka kwa kondakta,wahusika wa magari tofauti wakiwa kazini
katika barabara kuu ya Shinyanga –Tinde eneo la Nhelegani katika manispaa ya
Shinyanga.
Jeshi hilo la polisi pia limemfukuza kazi kuanzia Juni
12,2014 askari polisi EX.G.3829 pc Prosper Kayaya wa kazi za kawaida kwa kosa
la utoro jeshini ambapo askari huyo alijipa likizo.
Kamanda Kihenya amekemea vitendo hivyo kwani ni kinyume
cha mwenendo mwema wa jeshi la polisi huku akiwataka askari wa jeshi la polisi
mkoani Shinyanga kufanya kazi kwa uwazi,uaminifu na uadilifu mkubwa.
MJUMBE Sr
Post a Comment