Rais Uhuru Kenyata leo amelihutubia Taifa na kuelezea masikitiko yake pamoja na kutoa pole kwa familia zilizofikwa na misiba kwa mauaji yaliyotokea na amesema serikali itagharamia shughuli za mazishi ya waliokufa.

Rais Kenyatta amesema matukio hayo ya mashambulizi yalipangwa kiufundi na kitaalam, na kwamba haoni kama kundi la Al shabab linahusika, isipokuwa ni baadhi ya viongozi wenye lengo la kuwagawa Wakenya.

Amesema tayari baadhi ya viongozi wa serikali na usalama wanaosadikiwa kuhusika katika matukio hayo wamekwisha fahamika na watachukuliwa hatua ndani ya muda mfupi.