BINSLUM MBEYA CITY INAUZA KULIKO COASTAL
BinSlum ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili na Mbeya City wenye gharama ya Sh360 milioni ambapo kila mwaka timu hiyo itakuwa inapewa Sh180 milioni amesema majungu na fitina ndivyo vilivyomtoa Coastal Union ya Tanga.
BinSlum amesema kuwa; “Nimeondoka Coastal baada ya kuchoshwa na majungu ya uongozi kwa maana kule nilikuwa najitolea tu fedha zangu sasa waliniwekea maneno mengi ndiyo nikaona bora nipeleke fedha zangu Mbeya City.”
“Maneno hayo yalinichosha, nikaamua kwenda Mbeya, kwanza nitatangaza vizuri biashara zangu kwani. Mbeya City watatangaza betri za RB katika jezi zao,” alisema BinSlum.
Kampuni hiyo inayojishughulisha na uuzaji wa betri na matairi ya magari, pia ipo katika mchakato wa kuingia udhamini na timu za Ndanda FC ya Mtwara na Stand United ya Shinyanga ili kutangaza matairi yake ya Vee Rubber na Double Star.
“Bado tunazungumza na Ndanda na Stand ili niweze kuwadhamini nao lakini thamani yao haiwezi kuwa kubwa kama ya Mbeya City,” alisema BinSlum.

Post a Comment