VITAMBULISHO
vya kupiga kura nchini, vitatolewa upya kwa wananchi wote, ikiwa ni
sehemu ya mchakato wa kuboresha daftari la kudumu la wapigakura.
Mchakato huo wa kutoa vitambulisho upya, utakaotekelezwa Septemba mwaka
huu, utagharimu Sh bilioni 293 .
Tofauti
na vitambulisho vya awali vya karatasi vilivyotolewa kwa mara ya kwanza
mwaka 2004, vipya vitakuwa vya plastiki. Vimebadilishwa kutokana na
matumizi ya teknolojia mpya katika uandikishaji.(Martha Magessa)
Teknolojia
itakayotumika ni ya Biometric Voter Registration (BVR), ambayo
inachukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu
na kuzihifadhi katika Kanzidata (database) kwa ajili ya utambuzi.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema
hayo jana wakati akifungua mkutano kati ya tume na wahariri wa vyombo
mbalimbali vya habari, kuhusu uboreshwaji wa daftari la wapiga kura.
Alisema
katika uboreshaji huo, wapigakura wa zamani, kwa maana waliokuwa kwenye
daftari la sasa, watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha
kuchukuliwa taarifa zao hasa alama za vidole, picha na saini zao katika
mfumo mpya wa BVR na hatimaye kupewa vitambulisho vipya.
Alisema
vitambulisho hivyo vipya, vitatolewa papo hapo uandikishaji ukikamilika
na vitakuwa vya plastiki ngumu na namba ya mpigakura itakayoonekana
kwenye kitambulisho hicho, itakuwa ni ya kudumu na pekee kwa mpiga kura
husika.
“Vitambulisho
hivi vitatumika kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na kura ya
maoni ya Katiba mpya na kuhitimisha matumizi ya vitambulisho vya wapiga
kura vya awali,” alisema Lubuva.
Akiwasilisha
mada katika mkutano huo kuhusu maandalizi hayo kwa kutumia mfumo wa
BVR, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba alisema wapigakura
watakaokuwa na kadi za zamani, watatakiwa kwenda na kadi hizo katika
kituo cha kujiandikisha kurahisisha kuhamisha taarifa zao za awali
katika mfumo mpya.
“Hata
hivyo, kupotea ama kuharibika kwa kadi ya awali, hakumzuii mpiga kura
kwenda kituoni kujiandikisha na kupewa kadi mpya,” alisema.
Wenye
umri miaka 17 Alisema kundi lingine litakalohusika katika uboreshwaji
huo ni watu ambao ifikapo siku ya uchaguzi mkuu mwakani, watakuwa
wametimiza umri wa miaka 18.
Pia, wale
ambao hawakuwahi kujiandikisha katika madaftari yaliyopita kwa sababu
mbalimbali, watahusika katika uboreshaji wa daftari.
Alisema
baada ya kukamilika kwa uboreshwaji huo, daftari la awali litawekwa wazi
katika maeneo husika na tarehe za ukaguzi, zitatangazwa ili kila
aliyejiandikisha kwenda kukagua na kuona kama taarifa zake, zimeandikwa
na kuchukuliwa kwa usahihi.
“Kipindi
hicho pia kinatoa nafasi kwa wapigakura waliojiandikisha katika kata
kuweka pingamizi kwa wale watakaoonekana wameandikishwa katika daftari
lakini hawana sifa kama wasiokuwa raia au wasiotimiza umri unaotakiwa
kisheria,” alisema.
Alisema
matumizi ya mfumo wa BVR, yataweza kutoa majibu kwenye changamoto
zilizojitokeza katika mifumo mingine iliyotangulia na kuwezesha kuondoa
wapigakura, waliojiandikisha zaidi ya mara moja, kutambua wapigakura
siku ya uchaguzi na kuhamisha wapigakura waliohama.
BVR ni
uandikishaji tu Hata hivyo, Lubuva alisema mfumo huo wa BVR utatumika
kwa ajili ya kuandikisha wapigakura pekee na si kwa ajili ya kupiga kura
kielektroniki au vinginevyo.
Alisema
matumizi ya mfumo huo, yametokana na changamoto zilizojitokeza katika
matumizi ya Optical Mark Recognition (OMR) na kufanya daftari la kudumu
la wapigakura kuwa na kasoro na kusababisha wadau wa uchaguzi kuhoji
uhalali wake.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari, Lubuva alisema vifaa kwa ajili ya kazi
hiyo vimekwishaagizwa. Tume itavipokea Agosti mwaka huu ili kuanza
uboreshaji huo huku vifaa vichache kwa ajili ya mafunzo kwa watendaji
vitapokewa mwezi Julai na kuanza mfunzo hayo.
Uandikisha
kwenye vitongoji Alisema kwa sasa uandikishaji utafanyika katika ngazi
ya vitongoji, vijiji na mitaa, tofauti na awali ambapo vilikuwa katika
ngazi ya mtaa. Sasa vituo vya kujiandikishia, vimeongezeka kutoka 24,919
hadi 40,015 ili kuwa karibu na wananchi na kuongeza mwamko wa
kujiandikisha na kupiga kura. Mchakato wa uandikishaji ukianza, huduma
zitakuwepo kwa siku 14 kituoni.
Maandalizi
Alisema maandalizi ya awali yamekamilika, kinachofuata ni mafunzo na
kuanza uboreshwaji wa daftari utakaogharimu Sh bilioni 293 wanazopata
kutoka serikalini na tayari sehemu ya fedha, wameshapokea na kutumika
kukagua vituo .
Naibu
Katibu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Tehama, Dk Sist Cariah,
akizungumzia suala la vitambulisho vya taifa na hivi vya wapigakura,
alisema vitambulisho hivyo ni tofauti kwani wao wanatoa kwa ajili ya
kukamilika kwa muda maalumu lakini vile vya taifa ni endelevu.
Alisema
kwa sasa, vitambulisho vya taifa hawajakamilisha kutoa hata Dar es
Salaam pekee hivyo ni vigumu kutumika kwa uchaguzi ujao na kura ya maoni
kwa Katiba mpya lakini wakikamilisha vitambulisho vya taifa ,
vitatumika katika uchaguzi.
Alisema
katika mfumo huo mpya, watawasiliana na Wakala wa Usajili Ufilisi na
Udhamini (RITA) kuweza kuwaondoa wote waliofariki kwa kutumia takwimu za
hospitalini na vyeti vya vifo vitakavyotolewa.
Chanzo:Habarileo
MJUMBE Sr
Post a Comment