Unknown Unknown Author
Title: KIONGOZI WA CUF ALIYE SHAMBULIWA KWA KIPIGO NA WALIO JERUHIWA KWA RISASI WAWA TUHUMU ASKARI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Askari watuhumiwa kuwajeruhi wanawake wawili kwa risasi.  Askari wa jeshi la polisi wameshutumiwa kwa kuwajeruhi kwa risasi...

Askari watuhumiwa kuwajeruhi wanawake wawili kwa risasi.
 Askari wa jeshi la polisi wameshutumiwa kwa kuwajeruhi kwa risasi wanawake wawili na kumshambulia kwa kipigo kiongozi wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Kinondoni .
Kutokana na shutuma hiyo dhidi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni, ITV imefika katika hospitali ya Mwananyamala walikodaiwa kufikishwa watu hao watatu na kukutana kwanza na mkurugenzi wa ulinzi wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Kinondoni bwana Mwinyipembe Bakari akiwa amelazwa huku Bi Zawia Hamisi na Grace Loy walilalamikia kupigwa risasi wakidaiwa kuondolewa haraka katika hospitali ya Mwanayamala kutokana na usumbufu wa ujio wa vyombo vya habari,ambapo licha ya ITV kuangaika kwa zaidi ya masaa manne kuwatafuta na kuwakuta eneo la Kisiwani wakihudumiwa na ndugu zao ambapo katika mahojiano wamesema walikuwa wakisherekea shughuli ya ndugu yao na walijua kuwa sheria hazuii kufanyika sherehe mchana.
Diwani wa kata ya Makumbusho bwana Harubu Mohamed amesema wanawake hao walipigwa risasi huku ndugu zao nao wakija juu wakihoji kwanini askari walitumia nguvu kubwa kiasi hicho na kushindwa hata kupiga mabomu katika kutawanya watu hao? Daktari aliyehudumia wanawake hao dakta Thomson Minja amesema watu hao walipigwa na kitu chenye ncha kali na kusababisha matundu yenye kina kirefu katika baadhi ya sehemu ya miili yao huku kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni camilius wambura ambaye alikuwa kikazi nje ya ofisi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kikundi hicho cha kanga moko moko walikuwa wakifanya mambo ya aibu mbele za watu jambo ambalo sheria inazuia na kwamba bado uchunguzi unaendelea ili kuweka wazi kama walipigwa na kitu gani na askari yupi alihusika.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top