Wanawake wengi huamini kuwa uzuri wa maumbile ni jambo la muhimu sana kwa mwanaume jambo ambalo sio la msingi kabisa katika kujenga penzi linalodumu.Uzuri wa maumbile unaweza kumvuta mwanaume kuanzisha uhusiano lakini sio kitu ambacho kinaweza kuwa nguzo muhimu ya kudumisha uhusiano huo. Mwanaume anahitaji mwanamke ambae atakuwa chemchemu ya kudumu ya furaha katika maisha yake. Yafuatayo ni mambo kumi ambayo hunyausha penzi la mwanaume.
1. Kumpigia simu au kumtumia ujumbe mfupi (SMS) mara kwa mara na kulaumu pale ambapo mwanaume hapigi simu mara kwa mara au kutuma SMS. Siku hizi kuna SMS zilizotungwa ambazo zina maneno mazuri mazuri ya kimashairi na wanawake wavivu huzitumia hizo kuwatumia wanaume kuonyesha mapenzi yao, ukweli mara nyingi zinakuwa kero kwa wanaume kwa kuwa hazina uhalisia unaotoka kwa mtumaji. Wanawake wenye tabia hii hawajui umuhimu wa kumfanya mwanaume akumiss kwa muda fulani. Iwapo sitaki kukushirikisha ninavyoweza swali lako litanifanya nijisikie vibaya kwako nachukia kusema uongo hivyo nitakuchukia na kukuona kuwa unataka kunilazimisha kukueleza kila kitu kilicho moyoni mwangu.
2. KUKUBALIANA NA KILA KITU
Mwanamke ambaye anaogopa kuachwa, kufokewa na yuko tayari kufanya jambo lolote lile ili kumfurahisha mwanaume anaboa. Sio hilo tu bali inaumiza kuona kuwa umekuwa mpokeaji zaidi ya mtoaji na hali hii huzalisha uchungu na dharau ambayo haimsaidii mwanamke. Upo umuhimu wa mwanamke kuonyesha kuw nayeye ana mawazo mazuri kwa kukataa kukubaliana na kila kitu anachosema mwanaume.
3. KUTAKA KUJUA MAWAZO YA MWANAUME
Mwanaume anapokaa kimya sio kwamba amekasirika bali anapanga mambo yake na hataki kuingiliwa. Wanawake wengi waonapo mwanaume yuko kimya hukimbilia kuuliza “unawaza nini?” swali hili ni kero mbaya sana kwani unaingilia uhuru wa mtu mwingine. Tatizo hili linaenda pamoja na mwanamke mwenye tabia ya kutaka kwenda na mumewe kila mahali. Hali hii sisi wanaume tunachukia sana. Iwapo sitaki kukushirikisha ninavyowaza moyoni mwangu, swali lako litanifanya nijisikie vibaya kwani nachukia kusema uongo hivyo nitakuchukia na kukuona kuwa unataka kunilazimisha kukueleza kila kitu kilicho moyoni mwangu.
4. WASIOJISHUGHULISHA VYA KUTOSHA KITANDANI
Mchezo siku zote huhusisha pande mbili na katika tendo la ndoa ni hivyo hivyo. Asilimia 85 ya wanawake ni wavivu katika tendo la ndoa jambo ambalo ni kero kwa wanaume. Kwa kuwa wanaume wana tatizo la nguvu za kiume na kuwahi kumaliza mwanamke ambaye hajishughulishi wakati wa tendo la ndoa huzalisha hasira kwa mwanaume. Mwanaume afanyapo tendo la ndoa kwa ufanisi mzuri hasa akirudia zaidi ya mara moja anakuwa amepunguza makali ya kichocheo (hormone) cha TESTOSTERONE, kichocheo hicho kikipungua na hasira hupungua. Kutokana na ukweli huo uvivu wa mwanamke kitandani mara nyingi humkasirisha mwanaume. Kwa kuwa mwanaume huyo hawezi kumwambia mwanamke mapungufu hayo hasira hiyo hujitokeza katika maeneo mengine tofauti kabisa jambo ambalo huwashangaza wanawake wengi.
5. KUTUMIA TENDO LA NDOA KAMA SILAHA
Wanaume wote hupendelea tendo la ndoa hadi katika Biblia ikaandikwa “MSINYIMANE” (2 KORINTHO 7) wanawake kwa kufahamu udhaifu huu wa wanaume wamewanyima wanaume unyumba kwa manufaa yao na kutumia tendo la ndoa kama adhabu au njia ya kulazimisha mabadiliko upande wa mwanaume.Mtazamo na tabia hii hubomoa nyumba.
Post a Comment