Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi anatafutwa na jeshi la polisi
kwa madai ya kufanya matukio mbalimbali ya kiharifu likiwemo tukio la
hivi karibu kumnyonga hadi kufa dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Bahati
Husein mkazi wa Ulongoni A Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Akizungunza na paparazi wetu dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa
jina la Moshi Hussein alisema mtu huyo ambaye anatambulika kwa jina
moja la Godfrey, kabla ya kumuua dada yake alikuwa akimtamkia mara kwa
mara kwamba ipo siku atamuua.
“Tulikuwa tunaona kama utani maana alikuwa akisema suala la kumuua
mara kwa mara na siku chache kabla ya kumuua walikuwa na ugomvi ambapo
Godfrey alikuwa akimhisi dada yangu (ambaye kwa sasa ni marehemu)
anamahusiana na mwanaume mwingine hali iliyosababisha kaka aje na
kuwasuruhisha,” anaeleza Moshi huku akilia kwa uchungu.
Aliendelea kusema baada ya kusuruhishwa alionekana kuridhika na
kumtaka mkewe (marehemu) ampikie ugali ambapo marehemu alifanya kama
alivyoagizwa lakini usiku wake akambyonga hadi kufa.
“Baada ya kumuua aliondoka usiku huo huo na asubuhi alipiga simu kwa
ndugu akisema eti anataka kuongea na mkewe kwa hiyo mtu aende ampe simu
ili wazungumze wakati anajua nini amekifanya!” anasimulia Moshi.
Alipoulizwa wao walijuaje kama marehemu alinyongwa hadi kufa, Moshi
alisema baada ya kifo hicho walikwenda kuripoti kituo cha polisi
Stakishali ambapo kabla ya kujua kama ndugu yao ni marehemu walimchukuwa
na kumkimbiza katika Hospitali ya Amana ambapo mara baada ya madaktari
kumchukuwa vipimo iligundulika kuwa dada tayari alikuwa mfu.
“Tulipohoji chanzo cha kifo chake ndipo tulipoambiwa kwamba vipimo
vinaonyesha marehemu amenyongwa na shingo yake imevunjika mara mbili,”
alisema.
Aidha, akitoa historia ya mtu huyo anayetajwa kama jambazi sugu, kaka
wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Husein, alisema
kabla ya kutokea kwa tukio hilo Godfrey alikuwa akitumikia kifungo cha
miaka 20 jela kwa kosa kama hilo (la mauaji) na aliachiwa huru mwaka
jana kwa msahama wa rais.
“Hadi anakuja na kuishi na dada yetu bwana huyu alikuwa jela
akitumika miaka 20 kwa kosa kama hili. Kwa sababu huyu jamaa (Godfrey)
ni mtu mwenye wivu sana na chanzo cha kufungwa miaka 20 ilikuwa ni baada
ya kumfumania mkewe na mwanaume mwingine gesti ambapo aliwauawa wote na
kesi kwenda mahakamani na kukutwa na hatia na kufungwa miaka hiyo 20
leo kamuua dada yangu, ina niuma sana,” alisema Abdallah.
Aidha, mjumbe wa eneo hilo la Ulongoni A ambaye jina lake hakulikuweza kupatikana mara moja alithibitisha kutokea tukio hilo.
Jitihada za kumpata Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamanda
Mariathe Minangi hazikuzaa matunda baada ya simu yake kupokelewa na mtu
aliyejitambulisha ni mlinzi wake na kudai RPC yupo kikaoni. Jitihada za
kumtafuta RPC bado zingaliendelea kwa ajili ya kutolea ufafanuzi tukuio
hili.
Kwa undani wa tukio hili, sikiliza kipindi cha Hatua Tatu Habari Ndio
Hii siku ya Alhamisi tarehe 26/06/2014 hapa 100.5 times kuanzia saa
tatu asubuhi hadi saa sita mchana.
CREDITY BY TIMES FM
Post a Comment