Unknown Unknown Author
Title: TASWIRA PICHA:HUDUMA YA UPATIKANAJI WA MAJI YA BOMBA MLOWO,IMETELEKEZWA NA WAHUSIKA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani;Mwanamke akielekea Mtoni kuchota maji kama alivyo naswa na Kamera Yetu. Pichani juu ni Hali ya Mabomba ya Maji ilivyo sasa kat...
Pichani;Mwanamke akielekea Mtoni kuchota maji kama alivyo naswa na Kamera Yetu.

Pichani juu ni Hali ya Mabomba ya Maji ilivyo sasa katika Mji mdogo wa Mlowo Picha Ilipigwa Mtaa wa Kiwandani;Mlowo.

'Hakika;Huku ni Kukubali Kuongozwa na Mfumo Unao Kufirisi na Kukukandamiza/Kukudumaza Zaidi ili uendelee Kuupigia Magoti Mpaka Kifo Chako.'

Ndugu Zangu;
Kwa Mtazamo wangu Hakuna Uhusiano wowote kati ya nguvu iliyo tumika kusambaza miundo mbinu ya Maji Katika Mji mdogo wa Mlowo na Upatikanaji wa Maji wa Kudumu.
Hii ni kodi yangu mimi,wewe na Ndugu zetu wengine wa Kule Kijijini ime fujwa.Kusambaza Mabomba tu na Kutengeneza Intake Ni gharama kubwa ambayo ili hitaji kuwepo ulinzi wa kutosha kuanzia kwenye Chanzo hati kwa Watumiaji.Hili lingewezekana tu kama Utamaduni huu ungejengwa awali kwa jamii husika.
Lakini mambo ni Tofauti kabisa Tumechagua Kurudi tuliko toka! Kurudi kwenye maji ya Visima na ya Mtoni.Na wengine wame ichukulia hali ya Uwepo wa Maji ya Bomba kama Tishio la Ajira yao ya Maji ya Bomba maana kwao Mabomba kuto kutoa maji ni Neema kwani watauza ya kwenye Magaloni.
MWISHO:Wahusika Kumbukeni kuwa Mlitumia Gharama Kubwa sana Kutengeneza miundo mbinu ya maji katika Mji wa Mlowo;Lakini Mme itelekeza na kuisahau kabisa.
 MUNI NUKUU TAFADHARI;

"Hakika Mme Tumia Gharama kubwa sana kuwa kosesha Maji Wana nchi wa Mji Mdogo wa Mlowo,Mbozi!"

TAZAMA PICHA NA MAELEZO ZAIDI....
 

WANANCHI WA MLOWO WAMECHAGUA KUENDELEA KWA KURUDI NYUMA!

    Pichani:Nilipo kutana na watoto Wa Mji Mdogo wa Mlowo Wakiwa wanafuata Maji Kisimani,Baada ya Mabomba kung'olewa.
   Maji yakiwa Yanatiririka Kisimani nje kidogo ya Mji wa Mlowo
Pichani Maji yakiwa yana uzwa kwenye magaloni;Baada ya Maji ya Bomba Kuharibiwa


Nivema Kuhifadhi Mazingira yetu...
Ndiyo! Kwani Mazingira Mazuri ni Chanzo cha Afya.Pia Kuna Msemo kuwa Mji ni Uhai.Ilisemwa ilikuhamasisha jamii ijijengee Utamaduni wa Kuhifadhi Vyanzo vya Maji.

Lakini Kama Jamii ni vema Tuka kaa chini ili tu kujitathimini kiundani na kuujua Ukweli wa Ama Tuna Sogea Mbele,Tume Kwama au Tuna rudi nyuma?
Ndugu zangu,Wana Mlowo kwa kutazama Hatua tuliyo Fikia Mwaka 2010 na Leo 2015 katika Suala la Jamii kupata Maji kwa wakati na Uhakika Hali iliyopo Leo ni Ushahidi tosha kwamba Tumechagua Kusonga Mbele kwa Kurudi nyuma... Tuna Endelea kwa Kurudi tulikotoka!
Tumefika hapa si kwa mapenzi ya MUNGU Bali ni kwa Mapenzi Yetu wenyewe.
Hatuja Chelewa;kuanza Upya si UJINGA.Tuna weza Kujisahihisha.
Picha Zote Maktaba


MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top