Unknown Unknown Author
Title: MGOMBEA URAIS WA NCCR MAGEUZI ATOA TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA WA CHAMA CHA NCCR – MAGEUZI 17 Juni 2014. 1 :0    UTANGULIZI Ndugu wana habari na ndugu Wata...





TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA WA CHAMA CHA
NCCR – MAGEUZI 17 Juni 2014.

1 :0    UTANGULIZI
Ndugu wana habari na ndugu Watanzania, kwa kutambua mchango wangu
mkubwa ambao nimkuwa nikiufanya katika ujenzi wa vyama vya siasa hasa
Upinzani hapa nchini, ni dhahiri nimekuwa mjenzi wa vyama kuliko
mafanikio ya wananchi.  Nimegundua mengi sana na kujifunza mengi sana
juu ya hivyo vyama vyetu vya Siasa, tunapotafuta demokrasia katika
nchi yetu sio tu kuwa huru kwa kila jambo bali kuwa na UTU kwa watu

tunaowatafutia Demokrasia ya kweli, hatuwezi kusema nchi haina
demokrasia kama hatujatenda haki kwa wanachama au wananchi wetu.

SABABU ZA KUJIUDHURU UANACHAMA NA NYADIFA ZOTE ZA UONGOZI.

2 :0    AJALI YA GARI
Mwaka jana June 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa Udiwani Wilayani
sengerema Kata ya Nyampulukano na mimi nikiwa msimamizi wa Uchaguzi
huo mdogo wa marudio, jumamosi ya kuamkia uchaguzi tulipata ajali ya
gari tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura na mimi nilikuwa kiti cha
mbele cha gari na nikapata maumivu makali sana, japo nilipewa huduma
ya kwanza lakini baada ya hapo sikupata matibabu stahiki kitu ambacho
mpaka sasa, nisingeweza kulaumu kama hawajui lakini wanajua fika
viongozi wenzangu, na ukizingatia wakati ule nilikuwa Katibu wa
Mahusiano na Uenezi Taifa kitengo cha Vijana.

Kutokana na hali kuwa si nzuri na kufikia kuona nalalamika ujue kabisa
hali si nzuri ki afya, jambo la msingi kwa wenzangu hata kama wanahisi
na makosa lakini jambo la Busara ni UTU kwanza wakumponya aliye
mgonjwa ndipo busara zingine zinafanyika, kiukweli nasikitika sana na
ninaumia sana kwa tukio hili maana ile ilikuwa ni kazi ya chama na
siya mtu, ina maana hata Elfu kumi tu nayo ni ngumu ?  kweli hapa
tujiulize sasa, na ndio maana naumia sana kwa hilo, kwa hili mimi
naona kama wamenitelekeza na kuniachia familia yangu mzigo.

Nashauri tu kuwa vijana wenzangu wa Kitanzania tunapo jiunga na vyama
vya Siasa  tuchunguze UTU kwanza kabla hatujafikia maamuzi na tusiwe
washabiki wasiasa bila kujua hatima yetu kimaisha, nashauri kama
vijana tuwe tunasapotiana kwenye matatizo maana leo limemkuta Kisandu
kesho linakuja kwako.  Nimejaribu hatakuomba msaada kwa baadhi ya
viongozi rafiki msaada wa aina yoyote bila mafanikio.

USHAURI WANGU kwa chama changu NCCR – Mageuzi naomba kama hili
limetokea kwangu basi lisijirudie kwa mwingine kwani hata Mungu
hapendi kuona hali kama hizo.

Kutokana na hili la matibabu ndugu na familia yangu wamenishauri
niachane na Siasa za vyama ili waweze kuona wananisaidia vipi,
kimsingi naungana na ndugu zangu na kukubali ombi lao kuliko kuumia
namna hii.  Naomba msamaha kwa viongozi wenzangu pale tulipo kwazana
na mimi na wasamehe pale walipo nikosea japo nabaki na maumivu ya
kiafya.


3 :0    KATIBA MPYA
Kwa upande wa swala la KATIBA MPYA, huu mchakato si wa mtu mmoja au
watu kadhaa bali ni mchakato wa Watanzania wote.  Swala la Muundo wa
Muungano si swala la CCM wala UKAWA bali ni letu sote, hapa
ningeshauri tu kuepuka mvutano baina ya serikali mbili au Serikali
tatu, wakakaa pamoja na kufikia maridhiano yenye Busara ili tupate
Katiba mpya inayoendana na mazingira ya Kitanzania.   Pia lazima
wawakilishi wetu Bunge la Katiba watambue kuwa maoni ya Serikai mbili
ni ya Wananchi na Maoni ya Serikali tatu nayo pia ni ya Wananchi hivyo
Busara ndio itumike kurejesha Umoja wetu wenye katiba ya pamoja.

4 :0    KUHUSU BAJETI YA SERIKALI MWAKA  HUU
Viongozi wetu watambue kuwa Bajeti hii ni ya Watanzania wote hivyo
badala ya kukosoa tunapaswa kuboresha na tusikosoe bila kuiboresha
maana kama tutakosoa tu mwisho wa siku tutakuwa hatuja tibu chochote
bali serikali ikosolewe kwa kupewa solution.


5:0     UKAWA
Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi,  Baba au Mama akibagua
baadhi ya watoto tena wadamu ni dhambi kali sana ya ubaguzi
inayohitaji kukemewa.  Ndugu zangu wanao jiita UKAWA hawa jamaa si
wazalendo kabisa wametawaliwa na dhambi ya ubaguzi wa vyama.  Vyama
vya Siasa vipo 23, vyama 22 vikawa ni vyama vya Upinzani, iweje leo
wote ni wapinzani eti UKAWA iwe ya vyama vitatu vya upinzani fikiria
kama ni uchaguzi Mkuu, vyama vitatu kugombea uchaguzi haisaidii maana
hata robo haijafika. Ubaguzi uliofanywa na hawa jamaa hauvumiliki
kabisa na si vitendo bali ni Umoja ndani ya Mtengano.  Wakiweza
kuungana vyote vyama 22 vikawa UKAWA basi nitakuwa tayari kuendelea na
siasa na hata Serikali 3 nitaunga mkono lakini dhambi ya kubaguana ya
vyama  itaendelea basi ni heri Serikali 2 au 1 maana UKAWA ni ya vyama
vitatu na si ya wananchi maana ya UKAWA ya wananchi ni ya vyama vyote
22 vya Upinzani dhambi ya ubaguzi iacheni ni Pepo mchafu.


6:0     FIKRA MBADALA
Vijana wenzangu tuache mihemko na jaziba katika ushabiki wa mambo ya
kisiasa na tuhamie katika uzalendo wa kujenga nchi yeye Amani na
Uzalendo bila kujali itikadi za vyama vyetu na tusijikite kuchagua
vyama bali tuchague viongozi wanaotufaa bila kujali Ushabiki wa vyama.


7:0     MAPUMZIKO
Kwa sasa nimeamua kupumzika siasa na kuangalia mstakabli wa maisha ya
kifamilia kwanza, pamoja na kupumzika huko nitapumzika na kwamba
nitakuwa naelekea chama gani hilo si swala la leo mpaka pale
nitakapooona inafaa na sijui ni lini.

Ndugu wanahabari nifikishieni taarifa hii kwa umma wa Watanzania na
Mungu atupe uzima wa maisha marefu.

0786 025 609

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.


MWL. DEOGRATIUS KISANDU
ALIYEKUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA NCCR – MAGEUZI 17 / 06 / 2014

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top