picha ni rais wa Bugando na TAHILISO Mussa Mdede akiwa amepumzika kama alivyokutwa na mwandishi wa habari hii leo |
Kutoka kushoto ni kaka yake Mdede,katikati ni Mdede,alieshika simu ni waziri mkuuwa Bugando na mwisho ni rafiki wa karibu wa Mdede. |
Rais wa chuo kikuu Bugando Mussa Leonard Mdede amesema alitekwa na watu asiowafahamu siku ya jumatano ya tarehe 18/6/2014 majira ya jioni wakati akiwa katika maandalizi ya mwishomwisho kurudisha form ya kuwania urais wa chuo hicho kwa muhula mwingine,akiongea na mwandishi wa habari hii leo nje kidogo ya jijini la Mwanza ,bwana Mdede anasema licha ya kwamba hakumbuki lolote lile lililotokea,lakini anashawishika kuamini alitekwa na watu asiowafahamu kutokana na mazingira anayoendelea kusimuliwa na watu wake wa karibu.
Itakumbukwa kuwa taarifa za kutoweka kwa Mdede katika mazingira ya kutatanisha zilianza kusambaa tarehe 18 mwezi huu,ambapo taarifa za awali zilidai kwamba,Mdede alitoweka majira ya jioni wakati akijiandaa kurudisha form ya kuomba kuteuliwa kuwania urais wa chuo hicho kwa muhula mwingine,Mdede ambaye pia ni rais wa TAHILISO hakupatikana kuanzia tarehe hiyo mpaka jana usiku licha ya juhudi mbalimbali za kumtafuta kufanyika ikiwemo kulihusisha jeshi la polisi mkoa wa Mwanza,taarifa za kupatikana kwake zilianza kusambaa jana majira ya usiku,huku ikidaiwa aliokotwa na watu wasiofahamika eneo la Usagala lililopo jijini hapa.
Akiongea na mwandishi wa habari hii aliyemtembelea sehemu hiyo ambayo kwa sababu za kiusalama blog hii ya http://nicholauskilunga.blogspot.com/,haitafichua mahala hapo kwa kupataja,rais huyo alisema"kwanza ninamshukuru Mungu kwa kuwa watekaji wangu hawajanidhuru roho,lakini kimsingi sikumbuki lolote kuhusu utekwaji wangu ama kutoweka kwangu,nayoyakumbuka ni ya jumatatu ile,ila kwamba nilikuwa wapi,na kina nani ama nilifikaje hapa nyumbani sijui kabisa,kila nikijaribu kuvuta kumbukumbu zinakataa"alisema Mdede,hata aliendelea kusema hata hakumbuki kama alikuwa katika mchakato wa kugombea urais wa chuo huku akijiuliza watu waliokuwa wamemteka wamemfanyia kitu gani kilichomwondolea kumbukumbu kiasi hicho,kwani hana jeraha sehemu yeyote zaidi ya kusikia maumivu sehemu ya kichwa na maumivu ya mgongo,huku akisema anashindwa kumuhusisha mtu yeyote katika sakata hilo kutokana na kwamba katika siasa na uongozi ana maadui wengi ambao wanaweza kuwa wametokea katika kundi lolote kati ya hayo,kitu ambacho kinampa ugumu kuunganisha na kujua nani ama kinanani wamehusika kumteka.
Nae waziri mkuu wa chuo hicho Benjamini Thomas alisema ,anamshukuru Mungu rafiki yake na kiongozi wake amepatikana kwani alikuwa hana amani hasa kwa kuzingatia hali ya usalama hapa nchini si nzuri na matukio ya utekaji na kujeruhi yakiongezeka ,huku mamlaka husika zikishindwa kutoa majibu mujarabu,huku akiishukuru tume ya uchaguzi ya chuo hicho na uongozi wa juu kwa ujumla kwa busara yao ya kusitisha mchakato wa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike tarehe 29 mwezi huu.
Bwna Mdede alipoulizwa na mwandishi wa blog hii kama anatarajia kuendelea na harakati zake kisiasa na hasa kuhusu kuendelea na harakati zake za kugombea urais wa chuo chake cha Bugando,bwana Mdede alisema kwa sasa hawezi zungumzia mambo hayo,bali amejikita katika kuiangalia afya yake na kuiimarisha ili itengamae,na kwamba siasa zipo tu na zitaendelea kuwepo,lakini hajakatishwa tamaa hata kidogo,huku akiishukuru familia yake,viongozi wake wa Bugando,SAUT na vyuo vingine kwa kuchagiza utafutwaji wake.
Mdede alisema anahisi sababu kubwa ya maswahibu yanayompata ni kutokana na misimamo yake,na ndo anahisi imemponza,hasa katika kusimamia kile anachokiamini akiwa kama mwenyekiti wa TAHILISO na rais wa Bugando,huku kaka yake aliyeomba hifadhi ya jina lake anasema yeye anawatilia shaka watu walimleta mdogo wake nyumbani kwake kwani maelezo yao yanatia shaka,anasema "watu wale wanadai walimuokota mdogo wangu katika eneo la Usagala akiwa hajielewi na wakamchukua na kumpeleka Igoma,sasa hapa swali la kujiuliza ni kwanini waamue kwenda nae kwao Igoma na si kituo cha polisi ama hata kwa uongozi wa serikali ya mtaa?"alitoa wito kwa jeshi la polisi kufanya uchunguzi zaidi na kwamba wanaweza hata kubuni picha za watu wale waliompeleka mdogo wake nyumbani kwake.
mpaka mwandishi wa blog hii http://nicholauskilunga.blogspot.com/,anaondoka eneo hilo lenye ulinzi mkali,vipimo vya daktari vilikuwa haivijatoka na hivyo kushindwa kuelewa ripoti ya daktari itasema nini,hata hivyo Mdede alionekana bado afya yake haijatengamaa vizuri na huku alikuwa akiongea kwa unyonge na uchovu na zaidi mwandishi wa habari hii alishuhudia kwa jinsi suala la kumbukumbu linavyomsumbua kwani ilikuwa inamchukua mda kujibu swali na wakati mwingine ikimlazimu mwandishi wa habari hii kurudiarudia maswali.
Asante:Nicholaus Kilunga
MJUMBE Sr
Post a Comment