| Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa pembeni ya ndinga mpya aina Nissan Murano aliyoivuta ambayo thamani yake ni shilingi milioni 35. |
| Huu ni mjengo wa Nay wa Mitego uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 120. |
Wengi walimuona kama amevamia gemu bila kujipanga huku akielekeza nguvu
kubwa kuandika mashairi ya kuwaponda wasanii wenzake, wanasiasa na watu
maarufu huku akitangaza bifu na wasanii kibao.
Kumbe mchizi huyo anayependa pia kuitwa True Boy, alikuwa ameona mbali
na kuamua kutoka kwa staili ya kivyakevyake, akazidi kukomaa kwenye gemu
na kuzidi kujizolea mashabiki kibao waliokuwa wakiizimia kinoma staili
yake ya kuimba kibabe.
Ngoma ya Muziki Gani aliyofanya na Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ ikaleta mapinduzi makubwa katika muziki wake,
akaanza kupendwa hata na wale ambao awali hawakuwa wakimkubali.
Muvi likaendelea huku umaarufu wake ukizidi kupaa, akafunga kazi kwa
kuachia ngoma ambayo bado inaendelea ‘kubang’ mpaka sasa, Nakula Ujana.
Akapata shoo zisizo na hesabu na kubwa zaidi, akalamba mkataba wa pesa
ndefu kwenye kampuni moja ya simu za mkononi, na sasa anakula ujana
kinomanoma.
MJENGO WA MAANA
Ndani ya kipindi kifupi tu ambacho True Boy amepanda kwenye chati, tayari anamiliki mjengo wa maana uliopo Kimara Baruti jijini Dar ambao kwa mujibu wake, umegharimu zaidi ya shilingi milioni 120 (tazama picha), ukiwa na vitu kibao vya kisasa ikiwemo fensi ya umeme, CCTV Camera na fenicha za hatari.

“Mjini hakuna baba mwenye gari bali kuna baba mwenye nyumba, heshima
inaanzia kwenye nyumba, nilipopata mkwanja, jambo la kwanza lilikuwa ni
kwenye mjengo. Hii nyumba niliinunua kwa mtu ikiwa ya kawaida kabisa,
ikabidi niifumue na kuanza upya kujenga ili kupata kitu nilichokuwa
nakitaka.
“Najivunia sana kuwa na nyumba ya maana, hata kesho nikifa najua
nitazikwa kwangu. Ninazo nyumba nyingine kadhaa, Mungu akitujaalia mwezi
Oktoba nitaitambulisha nyumba yangu nyingine ambayo itakuwa
imekamilika,” alisema Nay wa Mitego.
MKOKO WA NGUVU, BAJAJ 2
Ukiachilia mbali mjengo huo ambao kwa mara ya kwanza Nay ameutambulisha kupitia Gazeti la Ijumaa, pia mchizi amevuta ndinga mpya, Nissan Murano ambayo thamani yake ni shilingi milioni 35.
“Nimenunua Nissan Murano mpya kutoka Showroom, nafikiri bei yake inafahamika, milioni 35 cash.

Pia nimenunua Bajaj mbili mpya kwa ajili ya wadogo zangu ziwe
zinawasaidia mambo madogomadogo. Kila moja nimenunua shilingi milioni 6.
Sitaki wadogo zangu wapate shida kabisa, nataka wajishughulishe.
“Namshukuru sana Mungu kwani sasa nayaona matunda ya jasho langu,
nawashukuru mashabiki na wadau wanaonipa shoo, najisikia furaha sana,
ukiwa na nyumbani kwako raha sana, namshukuru mama kwa kunifundisha
maisha na namshukuru pia demu wangu, Siwema,” alisema Nay.
Kufuatia mafanikio hayo makubwa aliyoyapata ndani ya kipindi kifupi, Nay
wa Mitego anaingia katika orodha ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya
wenye mafanikio makubwa. Big up True Boy!
Chanzo
GPL
PICHA ZAIDI....

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubofya LIKE Ukurasa wetu wa Fb.
MJUMBE Sr

Post a Comment