Mtoto
Melina wa (15) aliyefika katika Jiji la Dar es Salaam mwaka 2012
akitokea kijijini Ishozi- Kiziba, Kagera kwa lengo la kufanya kazi za
ndani, yaani ‘hausigeli’ akiwa amejeruhiwa vibaya na bosi wake
anayefahamika kwa jina moja la Yasinta.
SIKU 730 au
miaka miwili ya unyama na ukatili uliombatana na vipigo mfululizo,
vimempa wakati mgumu katika maisha mtoto wa miaka 15, Melina aliyefika
katika Jiji la Dar es Salaam mwaka 2012 akitokea kijijini Ishozi-
Kiziba, Kagera kwa lengo la kufanya kazi za ndani, yaani
‘hausigeli’Melina amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) ya Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar baada ya kujeruhiwa vibaya usoni na
kichwani na bosi wake anayetajwa kwa jina moja la Yasinta ambaye ni
mwanasheria mkubwa nchini.
Tukio
hilo la kusikitisha, lilijiri Ijumaa iliyopita nyumbani kwa mwanamke
huyo, Boko-Magengeni jijini Dar ambako Melina alikuwa akifanyia kazi.
Majeraha ya kichwani aliyopata mtoto Melina baada ya kupigwa na kwanja la kufyekea nyasi.
Binti
huyo ambaye wakati anafika jijini Dar alikuwa na miaka 12, licha ya
umri wake kuwa mdogo alifanya kazi kwa bidii ili mshahara wake uweze
kuwasaidia wazazi wake ambao hawajiwezi kimaisha kule kijijini.
SAKATA ZIMA LA MELINA
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, Melina alichukuliwa na bosi wake huyo kwa
makubaliano ya mshahara wa shilingi 40,000 kwa mwezi huku shilingi
20,000 zikitumwa nyumbani kwao Kagera.
“Lakini
katika hali ya kushangaza, bosi wake alikuwa hampi zile shilingi 20,000
kama makubaliano yao yalivyokuwa akisema kwamba anamtunzia kuepuka
matumizi mabaya.
“Ikaelezwa
kuwa, akiwa ndani ya kazi, binti huyo alijikuta akipata mateso makubwa
kama vile kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kwa madai ya kukosa,
kufanya kazi vibaya au tofauti na maelekezo,” kilisema chanzo.
Melina
akiendelea kuuguza majeraha akiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) ya
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar baada ya kujeruhiwa vibaya usoni
na kichwani na bosi wake.
BINTI MWENYEWE ANASIMULIA
“Nimechoka
sana ndugu zanguni, nimeteseka sana, nisaidieni nirudi kwetu Kagera.
Kosa dogo napigwa na blenda na nyaya za kompyuta. Ndiyo maana sehemu
mbalimbali za mwili hadi kichwani nina makovu kama hivi.
“Mara
hii ya mwisho nilipigwa na kwanja la kufyekea ndiyo majeraha haya.
Wakati akinitesa bosi wangu alikuwa akiniambia hakuna wa kumtisha.
Nisaidieni jamani, miaka miwili ya mateso mfululizo sasa nataka kurudi
kwa wazazi wangu japokuwa hawana uwezo tutaishi hivyohivyo tu. “
MAKOVU 73 KICHWANI, MWILINI
Mbali na majeraha mapya, mtoto huyo ana makovu (majeraha yaliyopona)
73 kichwani na mwilini mwake ambayo yote yanadaiwa yalitokana na adhabu
ya mashambulizi ya kudhuru mwili ingawa haikubainika kama ni kutoka kwa
bosi wake huyo au la!
SIKU YA TUKIO
Juni 11, mwaka huu, saa 3 usiku,
Melina alipelekwa katika hospitali binafsi iliyopo Mbezi, Dar akiwa na
majeraha makubwa kichwani.
Aliambatana na wanawake watatu, mama Betty, mama Winnie na mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Rwechungura.
Walisema wao ni majirani wanaoishi
karibu na binti huyo na walifika hospitalini hapo kwa lengo la
kumsindikiza na kujua nini kinaendelea.
DAKTARI NA MELINA
Habari zinadai kuwa, daktari
aliyekuwa zamu usiku huo alishtushwa na hali ya Melina kwani alikuwa
akitokwa na damu nyingi usoni na kichwani.
Aliwatoa wanawake hao nje na kumuuliza Melina nini kilimpata ambapo alijibu: “Nilianguka na ndoo ya maji.”
Daktari
alimbana sana ndipo akapasua jipu kwamba alikuwa amepigwa na bosi wake
na kwamba hata makovu mengine ni majeraha yaliyopona ambayo yalitokana
na kipigo cha mara kwa mara.
DAKTARI AOMBA NAMBA ZA SIMU
Ikadaiwa
kuwa, daktari huyo aliomba namba ya simu ya mmoja wa wale wanawake
lakini walikataa na kumuomba daktari atoe yake wao ndiyo wangempigia.
SAKATA LATINGA POLISI
Habari
zinazidi kudai kuwa, daktari huyo aliendelea kuokoa maisha ya Melina
kwa kumshona nyuzi karibu kumi na mbili katika maeneo yaliyopasuka
lakini kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, ilibidi aende kutoa
taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe.
“Polisi
walikwenda nyumbani kwa mwanasheria huyo, lakini katika hali isiyokuwa
ya kawaida walikuta nyumba haina mtu tena ikiwa wazi kwa usiku huo.
“Inasemekana
katika wale wanawake watatu waliompeleka Melina hospitali, mtuhumiwa
alikuwepo ila alitoroka baada ya polisi kuonesha nia ya kumkamata.
“Hali
ya Melina ilizidi kuwa mbaya. Alfajiri ya Juni 12, mwaka huu ilibidi
ahamishiwe kwenye Hospitali ya Mwananyamala ambapo alipokelewa na kupewa
matibabu. Hali ikazidi kuwa mbaya, akahamishiwa Muhimbili.
POLISI WAKIRI, WAMKAMATA MTUHUMIWA
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alikiri kutokea kwa
tukio hilo na kuongeza kwamba, mtuhumiwa alitoroka lakini Jumamosi
iliyopita alitiwa mbaroni maeneo ya Mbagala jijini Dar.
NI HAUSIGELI WA PILI
MJUMBE Sr
Tukio
la Melina ni la pili, wiki mbili zilizopita, hausigeli mwingine,
Yasinta Lucas alikumbwa na kadhia kama hiyo. Yeye alilazwa Hospitali ya
Mwananyamala akidaiwa kuteswa, ikiwemo kung’atwa meno na bosi wake kwa
kumtuhumu kutofanya kazi vizuri.
Bosi
huyo alishapandishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar,
Juni 12, mwaka huu na kusomewa mashitaka ya kujeruhi.
Post a Comment