Ndugu zangu,
Alfajiri ya kuamkia Jumapili ya kesho, Ivory Coast inacheza na Japan kule Brazil. Hata hivyo, hata kama watapata bahati mbaya ya kupoteza mchezo, wachezaji wa Ivory Coast hawana mashaka ya kurudi nyumbani na kuswekwa kwenye kambi ya jeshi kama adhabu.
Huenda si wengi wenye kukumbuka. Ni kwamba, mwaka 2000, Ivory Coast ilitolewa mapema kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika. Na Rais wa nchi wakati huo, Jenerali Robert Guei , alikasirika sana kiasi cha kuamuru, kuwa pindi watakapotua Ivory Coast, kikosi kizima cha timu ya taifa kipelekwe ndani ya kambi ya jeshi kikafundishwe uzalendo. Kwamba Rais aliamini kushindwa kwa Ivory Coast ni matokeo ya kukosa mioyo ya uzalendo.
Na kweli ikatokea, kikosi kizima kiliishia kuwekwa kambini jeshini na kufanyishwa kazi ngumu ikiwamo kuimba nyimbo za uzalendo.
Hata hivyo, mchezo wa soka nao una Rais wake, anaitwa Sepp Blatter, Rais wa soka alipopata taarifa kuwa wachezaji wake wamefungiwa kambini, basi, Sepp Blatter akatoa tamko kali dhidi ya Jenerali, rais wa nchi, kuwa kitendo chake ilikuwa ni kuingilia mambo ya ' Utawala wa soka wa Sepp Blatter'.
Wachezaji wale wakaachiwa huru, ni baada ya siku tatu ndani ya kambi ya jeshi.
Na Jenerali Robert Guei mwenyewe siku zake za kukaa madarakani zikawa zinahesabika, ilipofika mwezi Oktoba mwaka 2000, naye akapinduliwa!
Kila la kheri Ivory Coast dhidi ya Japan..
Maggid Mjengwa,
0754 678 252
IVORY COAST YAILAZA 2-1 JAPAN
Mabao ya vichwa ya Wilfried Bony na Gervinho yaliyopishana kwa sekunde 98 yameipa mwanzo mzuri Ivory Coast katika Kombe la Dunia baada ya kuilaza Japan 2-1 katika mchezo wa Kundi C mjini Recife, Brazil.
Tembo hao wa Ivory Coast walimuanzishia benchi Nahodha wake, Didier Drogba lakini ni kuingia kwake ndiko kulikuja sambamba na mabao hayo.
Nyota wa Japan, Keisuke Honda aliifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 16 kabla ya Ivory Coast kusawazisha kupitiakwa Bony dakika ya 64 na Gervinho kufunga la pili dakika ya 65. Mapema katika mchezo uliotangulia jana wa kundi hilo Colombia iliiaza 3-1 Ugiriki.
Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa: Barry, Aurier, Bamba, Zokora, Boka/Djakpa dk75, Tiote, Yaya Toure, Die/Drogba dk62, Gervinho, Bony/Konan dk77 na Kalou.
Japan: Kawashima, Uchida, Morishige, Yoshida, Nagatomo, Yamaguchi, Hasebe/Endo dk53, Okazaki, Honda, Kagawa/Kakitani dk86 na Osako/Okubo dk68.

MJUMBE Sr
Post a Comment