Akizindua
zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza aliwasisitiza Wakuu
wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmshauri na Watendaji wote katika
mkoa huo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Aidha,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson
Maimu aliwaomba wakazi wa Pwani wenye umri wa miaka 18 na zaidi
kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo kwa kufika kwenye vituo vya
usajili wakiwa na nyaraka zinazothibitisha uraia, umri na makazi yao
ambazo ni cheti cha kuzaliwa, kitambulishocha mpigakura, pasi ya kusafiria, leseni ya udereva, vyeti vya elimu, kadi ya bima ya afya na kadi ya mlipakodi.
Post a Comment