Baada ya juzi usiku kukamilisha usajili wa Dejan Lovren, Liverpool imeendelea kujiimarisha kwa kufanya usajili mwingine ambao umemuhusisha staa alieng’aa kwenye kombe la dunia 2014 akiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji.
Divock Origi mwenye asili ya Kenya ndio mchezaji mpya aliyejiunga na kikosi cha Brendan Rogers akitokea Lille ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa £10m ambapo hata hivyo kwa mujibu wa BBC, Divock Origi ataendelea kuwepo Lille kwa mkopo hadi 2015 atakapojiunga rasmi na Liverpool.
Origi (19) ambae ni mtoto wa Mike Okoth aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya (Harambee stars) amesaini mkataba wa miaka mitano lakini atabakia Lille kwa mkopo wa mwaka mmoja na atahamia Anfield msimu ujao.
Baba wa Origi akiongea na millardayo.com Kenya wiki iliyopita, alisema mwanae alianza soka toka akiwa mdogo na hakuona tatizo ndio maana alimruhusu afanye anachopenda ambapo kwenye sentensi nyingine Baba anasema tofauti na wengine wanavyoweza kudhani, Origi ni mzungumzaji wa lugha ya Kiswahili pia.
Milard ayo.com
Post a Comment