Watu wasiopungua 24 wamekufa kutokana na mkanyagano wa watu katika maonyesho ya muziki jijini Conakry nchini Guinea.
Serikali ya nchi hiyo imetangaza wiki moja ya maombolezo, baada ya kile ilichokiita "mkasa wa kusikitisha" kutokea katika tamasha la muziki wa rap wa kundi lijulikanalo kama Instinct Killers la Guinea.
Watu wengine kadhaa walijeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya polisi vilivyokaririwa na shirika la habari la AFP.
Tamasha hilo lilifanyika siku ya Jumanne katika ufukwe wa bahari wa Ratoma, kaskazini mwa Conakry.
Mamlaka zimesema "zimeshtushwa na mkasa huo wa kusikitisha uliosababishwa na mkusanyiko wa watu wengi katika shughuli hiyo ya sanaa," imesema taarifa kutoka ofisi ya rais.
Madaktari wamesema kulikuwa na mabinti 13 miongoni mwa waliokufa.
SALIM KIKEKE
Post a Comment