ZIJUE SABABU YA TANZANIA,AFRIKA KUSINI NA ZAMBIA KUTUMIA WIMBO WA TAIFA WENYE MELODI INAYO FANANA!
·
SABABU YA TANZANIA, AFRIKA KUSINI NA
ZAMBIA KUTUMIA WIMBO WA TAIFA WENYE
MELODI INAYOFANANA
Huenda ukawa umejiuliza swali hili kwa
kipindi kirefu lakini hujawahi kupata jibu.
Kwanini Tanzania, Afrika Kusini na Zambia
zinatumia wimbo wa taifa wenye melody
inayofanana?
Melody za wimbo huo ambao kwa Tanzania
unaitwa ‘Mungu Ibariki Afrika, zimetoka
kwenye wimbo uitwao “Nkosi Sikelel’
iAfrika”, neno la lugha ya Xhosa lenye
maana hiyo hiyo pia).
Wimbo huo ulitungwa mwaka 1897 na
Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu
kwenye shule ya misheni ya jijini
Johannesburg.
Wimbo huo ulianza kutumika kama wimbo
maalum wa hekaheka za ukombozi wa
Afrika na baadaye kuanza kutumiwa kama
nyimbo za taifa za nchi tano barani Afrika,
zikiwemo Zambia, Tanzania, Namibia na
Zimbabwe baada ya kupata uhuru.
Zimbabwe na Namibia zimepata nyimbo
zingine za taifa. Wimbo huo kwa sasa
unatumika Tanzania, Zambia na tangu
mwaka 1994 kama sehemu ya wimbo wa
taifa wa Afrika Kusini.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa Tanzania ndio
ilikuwa nchi ya kwanza kuanza kuutumia
wimbo huo kama wimbo wa taifa 1961
pale ilipokuwa Tanganyika na kuendelea
nao baada ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar mwaka 1964
Tafsiri ya mashairi ya awali yaliyokuwa kwa
lugha Xhosa kwenda Kiswahili ilifanya na
kundi la watu.
Wimbo unaotumiwa na Afrika Kusini hata
hivyo ni mchanganyiko wa “Nkosi Sikelel’
iAfrika” na “The Call of South
Africa” (unaojulikana kwa lugha ya Afrikaan
kama “Die Stem van Suid Afrika”).
20 April, 1994 ndipo ilipotangazwa
kwamba zote Nkosi Sikelel’ iAfrika na Die
Stem ziwe nyimbo za taifa za Afrika Kusini.
Wimbo uliounganishwa ulianza kufanya
kazi October, 1997, baada ya maneno ya
Kiingereza yalipoongezwa na wimbo
kupangwa upya na Jeanne Rudolph.
Enoch Sontonga !!!!? (MaGu As One)
Asante;Ndamo Sitta
MJUMBE Sr
Post a Comment