Unknown Unknown Author
Title: MTATIRO ASHANGAZWA NA SABABU ZILIZO TOLEWA MAGAZETINI KUHUSU UNG,ATUKAJI WAKE CUF;YEYE ASEMA AMEPUMZIKA HAJA NG,OKA! ZAID INGIA HAPA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
"SABABU ZA MTATIRO KUNG’OKA CUF" - Hii nimeinasa Tanzania Daima…………Inasema; SIRI ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Pr...
"SABABU ZA MTATIRO KUNG’OKA CUF" - Hii nimeinasa Tanzania Daima…………Inasema; SIRI ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba kufanya mabadiliko kwenye kurugenzi zake kwa kumng’oa Julius Mtatiro kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, imefichuka. Vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho, vinadai kuwa sababu ya kwanza imetokana na viongozi wakuu wa chama hicho taifa kumtaka Mtatiro asigombee nafasi yoyote. Inaelezwa kwamba Mtatiro aliandaliwa kisaikolojia kwamba hatarudi kwenye nafasi yake kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji wake. Sababu ya pili ambayo inatajwa na baadhi ya viongozi wa CUF ni kwamba kiongozi huyo kijana, anadaiwa kujihusisha na matumizi mabaya ya fedha hasa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga. Kwa mujibu wa habari hizo, sababu ya tatu inaelezwa kuwa Mtatiro alikuwa akifanya siasa za kitoto (siasa nyepesi), zilizokuwa zinawakera baadhi ya viongozi wa juu wa CUF. “Mtatiro sio kama amependa mwenyewe kuacha nafasi hiyo la hasha, ukweli ni kwamba aliandaliwa kisaikolojia kuwa nafasi hiyo hatoshi na inamlazimu atoke ampishe Sakaya ambaye anaweza akasukuma gurudumu hilo la chama,” kilieleza chanzo cha habari hizo. ______________________________________________________ Hii habari imenishangaza sana….Tanzania Daima nalo limegeuka kuwa gazeti la kuandika habari za kubahatisha namna hii…kwani hamna vyanzo vya habari sahihi???? nilitegemea UHURU ndo wahangaike kuandika habari zisizo na kichwa wala miguu ….tusubiri tena kesho watakuja sijui na sababu zipi. KUPUMZIKA KWANGU WADHIFA WA JUU NDANI YA CUF KUMEGEUZWA KUWA DEAL…..Nigawieni basi MGAO wangu mkishauza. Amekaririwa katika Ukulasa wake akijibu Tuhuma alizo tajiwa. SOMA MAJIBU ZAIDI.... Jackson Odoyo, Dar es Salaam ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro amesema kwamba yeye hawezi kuwa malaya wa siasa kiasi cha kubabaishwa na propaganda zinazo enezwa kwamba, ameamua kutogombea nafasi yoyote katika Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho kwa sababu ya tamaa ya uongozi. Akizungumza na Habarimpya.com Mtatiro amesema kwamba hakuwai kufikiri kwamba anauwezo wa kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wala nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho kwa sababu bado hana uwezo nani mchanga katika siasa, kwani hata umri wake bado ni mdogo sana hivyo hawezi kufikiria nafasi hizo kwa sasa. "Kuna propaganda zimeanza kuelezwa juu yangu mengi yanasemwa lakini mimi ndiyo najua sababu na sababu yenyewe ni kwamba nina majukumu ya kijamii na kifamilia ambayo yananikabili kwa sasa, niko masomoni ninatakiwa kuwa darasani muda wote wakati mwingine napaswa kuwa masomoni kuanzia asubuhi mapaka jioni, hivyo nisingeweza kufanya mambo mawili mazito kwa wakati mmoja"anasema Mtatiro na kuongeza:. "Mfano nilikuwa na nafasi ya kushinda katika nafasi yangu ya Naibui Katibu Mkuu, lakini ni nafasi ambayo inamtaka mtu kwenye muda wa kutosha kuitumikia Chama, hivi sasa CUF inajiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za mitaa,na Uchaguzi Mkuu, namimi nitatakiwa kuwa masomoni mpaka mwezi July mwakani, hivyo nisingeweza kuitumia Chama ipasavyo. Mtatiro amefafanua kwamba kama kuna watu wameanza kuvumisha kwamba anaweza kuhamia vyama kama ACT na vingine wanajidanganya kamwe hawezi kuharibu kiwango chako cha uongozi, amejifunza mambo mengi kutoka kwa Profesa Lipumba na Maalim Sefu na kamwe hakuwai kugombana na viongozi hao hata siku moja. Asante Habari Mpya.com MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top