Unknown Unknown Author
Title: LUDEWA,AMANI:MAKABURU WAFUKUZWE AMA WAJE TUONGEE NAO HAPA KWANZA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni Mwonekano wa Eneo wanalo chimba Madini makabulu Kijijini Amani,Ludewa,Njombe Ni Takribani miaka mitatu sasa tangu Kampuni la uc...
Pichani ni Mwonekano wa Eneo wanalo chimba Madini makabulu Kijijini Amani,Ludewa,Njombe Ni Takribani miaka mitatu sasa tangu Kampuni la uchimbaji wa madini aina ya Dhahabu kijijini Amani,Ludewa lianze kuchimba madini hayo, Katika Mkutano wa kijiji wana nchi walionesha kuto ridhishwa na mwenendo wa Kampuni hilo kuto kuwa jali na kupuuza wito walio pewa mara kadhaa ili wakae na wana nchi na waafikiane katika masuala ya Ujenzi wa baadhi ya miundombinu na uchangiaji wa michango mbalimbali ndani ya jamii ya Amani. Wakiongea na viongozi wao wananchi wali dai mrejesho wa barua ya awli waliyo ituma kwa kampuni hilo la makaburu ambapo ili bainika kuwa walipuuzwa na madini bado yana endelea kuchimbwa na kusafirishwa kama kawaida. Kiongozi mmoja wapo aliye julikana kwa jina Moja la Method Luoga,alikiri kuwa Barua waliipeleka lakini hakuna Mrejesho walio pewa kama kijiji suala ambalo lili wakasirisha wana kijiji na kutoa agizo kuwa kama Kampuni hilo la uchimbaji madini lita puuza wito wao,basi listishwe kuendea na Uchimbaji kwa sababu hawa oni faida wanayo ipata kama wanakijiji kutokana na shughuli yao. Picha Na Taarifa na Mdau wa MJUMBE BLOG Aliye Amani,Ludewa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top