MAELEZO NA PICHA:UHAMIAJI WAWANASA NANE NA PASSPOT BANDIA UWANJA WA NDEGE NYERERE!
1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
2. SAMER HELMI KAMIT - SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI - IRAQ, PPT. NO. G 1111623
SOMA ZAIDI,,,,,,,,
Idara ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere, wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya. Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la Uturuki yenye Namba TK 603, wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa Raia wa Sweden na Belgium.
Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.
kukamatwa kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji haramu nchini ambapo suala la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele. akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji wanaendelea kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha Sheria na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa.
Post a Comment