MCHAKATO WA KATIBA WAINGIA DOSARI:BADO SAINI 10000 TU BUNGE MAALUM LIBURUTWE KWA PILATO!
Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila
Joto la kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba (BMK), linazidi kupanda nchini baada ya wabunge na vyama vya siasa kuendelea kusisitiza kuwa Bunge hilo halina tija kwa taifa.
Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amesema ameanza kukusanya saini za Watanzania wanaopinga kuendelea kwa Bunge hilo ili kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania, kusitisha vikao vinavyoendelea mjini Dodoma.
Mchungaji Mtikila akizungumza na Mwananchi Jumapili alisema mchakato wa kukusanya saini hizo unaendelea katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Geita, Kagera, Dar es Salaam huku akibainisha kwamba mwitio wa watu ni mzuri.(P.T)
"Natafuta saini 20,000 za Watanzania na sasa tayari tumekusanya saini zaidi ya 10,000 katika mikoa kadhaa na natarajia Watanzania wataendelea kuniunga mkono ili kuhakikisha mchakato huu. Nakwenda kuuzuia Mahakama Kuu na ninajua tu nitashinda," alisema Mchungaji Mtikila.
Alisema anakusanya saini hizo ili kudhihirisha kuwa Watanganyika hawataki muungano, kwani mwaka jana Wazanzibari walikusanya maoni 1,946 ya kupinga muungano.
Dk Chegeni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Dk Raphael Chegeni alisema kuendelea kwa Bunge hilo bila kuwepo kwa Ukawa ni kuchezea fedha za umma.
Dk Chegeni alisema hayo jijini Arusha alipokuwa akihudhuria vikao vya Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kwamba kuendelea na Bunge hilo ni kucheza kamari ya hatari ambayo baadaye inaweza kusababisha malalamiko kwa wananchi na kuwagawa wananchi.
"Sioni sababu ya haraka, huwezi kuandika katiba bila ya maridhiano, haya mambo yenye utata itabidi yapatiwe muda mwafaka na mchakato huu kuendelea baada ya uchaguzi mkuu mwakani."
Dk Chegeni alisema, kwa kuwa kuna mahitaji ya haraka yanayopaswa kuingizwa katika Katiba, ni busara Bunge la Novemba kutumika kufanya mabadiliko hayo, ambayo ni pamoja na kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, kuruhusu mgombea binafsi na pia kuingiza masuala ya haki za binadamu kwenye Katiba.
Alisema hadhani kama kuna haraka sana wa kuandika katiba wakati kuna kutoelewana, kwani Katiba inaweza kuandikwa hata na utawala ujao, ingawa nia nzuri ya Rais Jakaya Kikwete ilikuwa ni kuwaachia Watanzania Katiba Mpya.
Akizungumzia malumbano juu ya watu wanaotoa maoni ya mchakato wa Katiba nje ya Bunge hilo, alisema wanapaswa kuachwa kwani ni haki ya kila Mtanzania kutoa mchango wake ili kuwezesha kupatikana Katiba mpya.
Soma zaidi>>>>>>>>>>>
Post a Comment