Unknown Unknown Author
Title: PICHA NA MAELEZO:WANA KIJIJI CHA MBONGO LUDEWA WAME MTUMA ;FILIKUNJOMBE KUDAI HUDUMA ZA JAMII NA WALA SIO KATIBA MPYA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi wa kijiji cha Mbongo Manda Ludewa wakiwa katika mapokezi ya mbunge wao mida ya saa 5 usiku Wananchi wa Mbongo wakimkabidhi m...
Wananchi wa kijiji cha Mbongo Manda Ludewa wakiwa katika mapokezi ya mbunge wao mida ya saa 5 usiku
Wananchi wa Mbongo wakimkabidhi mbunge Deo Filikunjombe zawadi baada ya kufika kijijini hapo na kulala katika zahanati WANANCHI wa kijiji cha Mbongo wilaya ya Ludewani mkoani Njombe wakesha usiku kucha kufurahia mbunge wao Deo Filikunjombe kuwa kiongozi wa kwanza toka nchi ipate uhuru mwaka 1961 kufika kulala katika kijijini hicho. Wananchi hao walifika hatua hiyo jana baada ya mbunge huyo kufika kijijini hapo kutekeleza ahadi zake mbali mbali kwao ikiwemo ya kulala katika zahanati ya kijiji hicho kutokana na kutokuwepo nyumba ya kulala wageni Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja kati ya wananchi wa kijiji hicho John Haule alisema kuwa hatua ya wananchi hao kulazimika kukesha nje ya zanahati hiyo ni kutokana na maamuzi ya mbunge wao Filikunjombe kuamua kulala kijijini hapo ardhini jambo ambalo kwao wanaona kama ni miujiza hasa ukizingatia kuwa hakuna kiongozi hata mmoja wa wilaya ,mkoa ,Taifa hata kata aliyefika kijijini hapo na kuamua kulala kama alivyofanya mbunge huyo. Hivyo alisema mbali ya kuwa zipo sikukuu nyingi ila wao kufika kwa mbunge huyo na msafara wake kijijini hapo na kuamua kulala ni sherehe kubwa kuliko zote na wanamuona mbunge huyo kuwa ni mwakilishi wao wa kweli. “Ludewa tumepata kuwa na wabunge zaidi ya watano hadi sasa ila hakuna mbunge aliyepata kuzika katika kijiji chetu na kuamua kulala na wananchi hapa kijijini zaidi ya mbunge wetu huyo Deo Filikunjombe …..kweli tunasema kwa Ludewa hatutakuja kumpata mbunge kama yeye ila sisi kama wananchi wa kijiji cha Mbongo tunasema hatuhitaji mbunge mwingine zaidi ya Filikunjombe” Kwa upande wake Mbunge Filikunjombe akiwashukuru wananchi hao kwa kukesha usiku kucha alisema kuwa amepata kuzunguka vijiji vyake zaidi ya 70 vya jimbo hilo ila hajapata kukutana na mapokezi makubwa kama haya kiasi cha wananchi kulazimika kulala nje kwa furaha ya mbunge wao. Mbunge huyo alisema kuwa kwa vile nafasi hiyo ya ubunge anaipenda kamwe hatawaangusha wananchi wa jimbo la Ludewa katika utendaji wake na kuwa siku zote mbunge atahakikisha anawatumikia vema wananchi badala ya kulala kama wanavyofanya baadhi ya wabunge katika bunge hilo. “ Ndugu zangu wapiga kura wangu mimi si mbunge wa kwenda kusinzia bungeni ni mbunge wa kuwawakilisha wananchi wangu …..hivi mimi kwa kero hizi za wana Ludewa nikasinzie bungeni nimefurahia na nini ..nasema kamwe sitawaangusha wananchi wangu” SOMA ZAIDI KUTOKA KWA HUYU SHUHUD WETU..... Kawauliza Wananchi wake wa jimbo la Ludewa kwamba, Yeye Hajaenda Bungeni kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa Sabb ya kutatua matatizo mbali mbali kwenye Jimbo lake, Kawauliza Shida yao ni Katiba au Maji? Wananchi wakajibu Shida yao ni Maji.. i.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top