Unknown Unknown Author
Title: SINTOFAHAMU:MAITI YA OPOLEWA MTOONI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Friday Simbaya, Iringa WAKAZI wa Manispaa ya Iringa walijitokeza kwa wingi katika mto Ruaha mdogo kushuhudia mwili wa kijana wa jinsia y...
Na Friday Simbaya, Iringa WAKAZI wa Manispaa ya Iringa walijitokeza kwa wingi katika mto Ruaha mdogo kushuhudia mwili wa kijana wa jinsia ya kiume ukiwa umeelea juu ya maji ya m to huo huku Jeshi la Zima moto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani hapa kuuopoa mwili ukiwa umeharibika vibaya. Baada ya jeshi la uokozi kuopoa mwili huo waliuweka pembeni ya m to huo na kisha kuukabidhi kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi. Kijana huyo ambaye hakufahamika kwa jina wala makazi yake alizikwa kandokando ya mto. huo baada ya kukosekana kwa ndugu zake. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani iringa Ramadhani Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 10:00 Jioni eneo la ipogoro lililopo ndani ya manispaa ya iringa. Kamanda mungi alisema kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa hauna nguo huku akibainisha kuwa marehemu anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 20 hadi 30. Baada ya kuopolewa kwa mwili huo polisi kwa kuyshirikiana na jeshi la uokozi pamoja na vikosi vya ulinzi waliitisha mkutano wa utambuzi ili kama atajuikana aweze kuchukuliwa na ndugu zao lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza. Hata hivyo polisi hao waliiamua kuzika mwili huo pembezoni mwa mto huo huku mwili huo ukiwa umeharibika vibaya. "Ni kweli tulipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na tulifika eneo la tukio na hatimaye kwa kushirikiana na jeshi la uokozi tulimuokoa japo kijana huyo hakuweza kufahamika jina wala kabila na sisi polisi hatuna taarifa yeyote ya mtu kupotea."alisema mungi Wakati huo huo mashuhuda waliliambia MJENGWABLOG kuwa kitendo cha jeshi hilo kuzika mwili huo pembezoni mwa mto huo sio vizuri kutokana na mto huo kutumiwa na wakazi wengi wa manispaa ya iringa. Mashuhuda hao ambao hawakupenda majina yao yaandikwe walisema kuwa jeshi hilo lisingetakiwa kuzika eneo hilo badala yake wangetafuta eneo lingine kwa ajili ya maziko licha ya mwili huo kuwa umeharibika.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top