soma hapa:MJENGWA ATOA NJIA RAHISI YA KUPATA JAWABU LA MAISHA KWA WATANZANIA!!
Ndugu zangu leo nayaandika haya nikiwa Iringa mjini baada ya kusafiri kwa takribani siku saba sasa, nimejionea na kujifunza mengi kupitia safari yangu, japo natumia nafasi hii kuwapa pole wale wote walipata maafa kwa kuezuliwa nyumba zao kwa mvua ya upepo iliyonyesha jana jioni Mkoani Singida ambapo nilishuhudia tukio hilo hiyo jana kabla ya kuanza safari ya kurejea Iringa hii leo.
Pichani ni Dodoma ukiwa unaelekea Mtera baada ya kupita Dodoma Mjini, nyumba hizi wanazoishi watanzania ambao mgao wa Fedha za IPTL kupitia Escrow Account wao haukuwahusu, inasikitisha na kuhuzunisha miaka 53 ya Uhuru bado watu wanaishi kwenye nyumba ambazo paa lake ni la udongo, Japo Asili ni nzuri lakini ikipitiliza inakera bora kukomaa na Asilia.Nyumba hizi hazina tofauti na zile nilizoweka juzi Jimbo la Iramba Magharibi na maeneo mengine ya Mkoa wa Singida na Dodoma ambapo ni kama mahali pake pa nyumba za aina hizi ambazo ni Asili lakini si haba.
Naam, maisha haya nayafananisha na ile njia ya kupata jawabu wakati wa kufanya hesabu za MAGAZIJUTO

Post a Comment