NA KAROLI VINSENT
BARAZA la Mitihani nchini NECTA
limetangaza matokea ya kidato cha pili
yaliyofanyika mwaka jana 2014 huku idadi
kubwa ya wanafunzi wakiwa wamefaulu na
kujiunga kidato cha tatu, ikiongeza kwa
asilimia 92.66 ikilinganisha na mwaka 2013
ambapo idadi ya wanafunzi waliofaulu
ilikuwa asilimia 89.34.
Matokeo hayo yametangazwa leo Jijini
Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Baraza
la Mitihani nchini NECTA Dkt Charles E
Msonde wakati wa mkutano na waandishi
wa Habari ambapo alisema watahiniwa
waliofanya mtihani huo uliofanyika mwezi
Novemba mwaka jana ilikuwa 405,204 sawa
na asilimia 89.40 Kati ya hao wasichana
walikuwa 233,834 sawa na asilimia 51.60 na
wavulana walikuwa 219,357 sawa na
aslimia 48.40.
Dkt Msonde alisema kati ya watahiniwa hao
waliofaulu na kupata alama na kuweza
kuendelea na kidato cha tatu walikuwa
375,434 Sawa na asilimia 92.6 ya watahiwa
wote waliofanya mtihani huo ambapo
wasichana walikuwa 195,328 sawa na
asilimia 92.8 na wavulana 180106 sawa na
aslimia 92.69.
Aidha,Dokt Msonde aliwataja watahiniwa
ambao wamepata alama ambazo hawawezi
kuendelea na kidato cha Tatu na
itawanalazimu kurudia kidato cha pili
walikuwa 29770 kati ya asilimia 7.34.
Vilevile ,Dokta Msonde aliyetaja
masomo waliofanya vizuri wanatahiniwa
hao ni ya
Uraia,Historiya,Kiswahili,kingeleza,jeografia.
Pia Masomo waliofanya vibaya watahiniwa
hao ni ya Hesabu,Kemia,kilimo,Somo la
Biashara pamoja na Biolojia.
Alibanisha kuwa sababu iliofanya idadi ya
wanafunzi mwaka huu kuwa mazuri
imetokana na mipango mizuri ya serikali
huku ikizingatia sasa kuwepo na mfumo
mpya wa matokea mkubwa sasa na
akawata walimu na wazazi waendele kutoa
mshikamano kwa walimu.
Matokeo yote ya Kidato cha pili yatakuwepo
kwenye Mtandao wa baraza la Mitiani
nchini,tovuti ya Wizara ya Elimu na Ofisi ya
Wzari Mkuu Tamisemi, pamoja na Kwenye
shule husika ya Mwanafunzi anayesoma.
Timu yetu ya MJUMBE BLOG itawaletea Matokeo hayo pindi yatakapo wekwa mtandaoni;
Endelea kututembelea.
Sdcvbbv
posted from Bloggeroid
Post a Comment