Unknown Unknown Author
Title: IJUE SABABU YA UKAWA KUSUSIA KUSHIRIKI MCHAKATO WA KURA YA MAONI APRIL ,30,2015
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetangaza rasmi kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya k...

Dar es Salaam. Vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
vimetangaza rasmi kutoshiriki katika
mchakato wa kura ya maoni ya katiba na
kwamba kuanzia sasa vitahamasisha
wananchi kuunga mkono.
Uamuzi huo umetolewa leo na wenyeviti
wa vyama wanaounda umoja huo wa
ukawa ambao ni Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF,
Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia na
Mwenyekiti wa NLD, Makaidi.
Akizungumza wakati wa kutoa msimamo
huo Profesa Lipumba amesema wamefikia
uamuzi wa kutoshiriki katika zoezi hilo
kwa sababu mchakato mzima haukuwa na
maridhiano ya kitaifa.
"Vyama vya siasa ikiwemo CCM
vilikubaliana mwaka jana kwamba zoezi la
kura za maoni lifanyike mwaka 2016
baada ya uchaguzi mkuu, tulisaini wote na
Rais Jakaya Kikwete alikubali, kwa nini
mabadiliko yafanyike ghafla" amehoji
Profesa Lipumba.
Amesema jambo la kushangaza, Rais
Kikwete aligeuka na kutangaza kwamba
Aprili 30, mwaka huu kuwa siku ya kupiga
kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya.




Tutembelee MJUMBE BLOG mtandaoni kila mara upate Picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu na matukio mbali mbali yaliyo gonga vichwa vya habari nje na ndani ya nchi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top