Gazeti la The EastAfrican lapigwa marufuku
Tanzania
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku
kuchapishwa na kusambazwa kwa gazeti la kila
wiki la The EastAfrican kwa madai ya kuwa
halijasajiliwa nchini humo.
Hata hivyo Wilfred Kiboro, mwenyekiti wa
kampuni ya Nation Media Group, wachapishaji wa
gazeti hilo la lugha ya kiingereza, ameeleza kuwa
adhabu hiyo haikutarajiwa na wala haistahili na
kubainisha kuwa wamekuwa wakisambaza gazeti
hilo Tanzania kwa miaka 20 bila matatizo.
Kampuni ya Nation imedai sababu kubwa huenda
ni serikali ya Tanzania kutofurahishwa na
msimamo wake wa kuandika habari dhidi ya
maovu kama rushwa na kero nyingine nchini
Tanzania.
Kampuni hiyo imesema serikali ya Tanzania
imetaja kutofurahishwa na kibonzo
kilichochapishwa katika toleo la wiki hii, ambapo
imesema kimemdhalilisha Rais Jakaya Kikwete.
Hata hivyo BBC haikuweza kumpata afisa wa
serikali ya nchi hiyo anayehusika na usajili wa
magazeti kuweza kutoa maelezo zaidi.
"... Kuna kibonzo kimechorwa ukurasa wa 18 chapisho
la January 17-23 na kumtaja JK moja kwa moja
kitu ambacho si sawa, kumdhalilisha rais. Ingawa
wanasema sababu ni halina kibali na limekuwepo
nchini kwa miaka ishirini!!!??? Sijui kwa kweli!!??
Kwa Mimi nafikiri hiyo inaweza kuwa sababu, kwa
gazeti kubwa kama hilo kukosa kibali cha kuuzwa
nchini ni jambo ambalo haliwezekani. Yaani
unataka kusema maraisi wote waliopita
hawakuona hili suala!!?? Basi serikali hii iko makini..."
Alisema Mchangiaji Mmoja wapo katika moja ya mitandao ya kijamii nchini.
Tutembelee MJUMBE BLOG Mtandaoni kwa picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu,Matukio yanayo gonga vichwa vya habari ndani na nje ya nchi kila mara.
Post a Comment