Unknown Unknown Author
Title: JAJI WARIOBA ACHANGIWA NAULI KWENDA MVUNJO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Moshi, Kilimanjaro. Wananchi wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro wamechanga Sh200,000 za nauli ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko...



Moshi, Kilimanjaro.
Wananchi wa Jimbo
la Vunjo mkoani
Kilimanjaro wamechanga
Sh200,000 za nauli ya
Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba ili aweze
kufika jimboni humo kutoa
somo la Katiba.
Fedha hizo zilitolewa juzi
na kukabidhiwa kwa
Mwenyekiti wa NCCR-
Mageuzi, James Mbatia
wakati akihutubia mikutano
ya hadhara kwa nyakati
tofauti katika miji ya Himo
na Moshi Mjini kwa lengo
la kuwashukuru wananchi
kwa kuwaamini wagombea
wa Ukawa na kuwapa
ushindi katika Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano ya fedha
hizo, Katibu wa Umoja wa
Wanawake wa NCCR-
Mageuzi, Getrude Pwila
alisema kama hazitatosha
kwa nauli ya Jaji Warioba,
wako tayari kuchangishana
kuongeza.
“Tunataka tuelimishwe hii
Katiba Inayopendekezwa
kwa sababu hatuko tayari
kuipigia kura kwa sababu
hatuielewi, hatujaiona wala
kuisoma na kuielewa,”
alisema Pwila kwa niaba ya
wananchi wa jimbo hilo.
Katibu huyo, alimwomba
Mbatia ambaye pia ni
Mbunge wa Kuteuliwa,
amwombe Jaji Warioba
kwenda katika jimbo hilo
kuendesha kongamano
kama alivyofanya katika
miji ya Mwanza na Dar es
Salaam na wao wako tayari
kumgharimia.
“Leo tunayo nusu ya nauli
(Sh200,000) akikubali tuko
tayari kuchangia na kujazia
Sh200,000 nyingine na
tunakukabidhi shati la
kitenge kama alilokuwa
anavaa Mandela (Nelson) ili
ukamkabidhi,” alisema.
Pwila alisema wananchi wa
Vunjo wanamchukulia Jaji
Warioba kama Mandela wa
Tanzania, ndiyo maana
wamempatia shati hilo.
Jaji Warioba alipoulizwa
kuhusu maombi hayo,
alisema hajayapokea na
hajui lolote.
Katika mkutano huo, pia
wananchi walimkabidhi
Mbatia suti mpya ambayo
wanataka aivae
atakapokwenda bungeni
kuapishwa akiwa mbunge
wa jimbo hilo.
Mbatia awasha moto
Kwa upande wake, Mbatia
ambaye pia ni Mwenyekiti
mwenza wa Ukawa,
alimtaka Rais Jakaya
Kikwete kutekeleza
masuala aliyokubaliana na
viongozi wa vyama vya
siasa kupitia Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD)
mwaka jana.
Mbatia alisema moja ya
makubaliano hayo yalikuwa
ni kufanya mabadiliko ya
Katiba ya sasa ili kuruhusu
kuwapo kwa tume huru ya
uchaguzi ili Uchaguzi Mkuu
wa Oktoba uwe wa huru na
wa haki.
Vilevile, mabadiliko hayo
yangeruhusu kuwapo kwa
mgombea binafsi, matokeo
ya uchaguzi wa rais
kuhojiwa mahakamani,
mshindi wa urais kupata
zaidi ya asilimia 50 ya kura
na kuahirisha kura ya
maoni hadi mwaka 2016.
Akihutubia mkutano katika
Mji mdogo wa Himo,
Mbatia alisema mwaka huu
hawako tayari kuona
Uchaguzi Mkuu
unavurugwa na wasimamizi
wanaopokea maelekezo ya
Serikali. “Ninamwomba
Rais asimamie maridhiano
haya kwa masilahi mapana
kwake na kwa nchi yetu
kabla miezi yake hii minane
aliyobakia nayo haijawa
michungu kwake,” alisema.
Mbatia alisema
makubaliano hayo yalikuwa
ni ya utu na kwamba kwa
utafiti alioufanya anaona
giza mbele na hakuna
uwezekano wa kupitishwa
kwa Katiba
Inayopendekezwa kwa vile
haina maridhiano.
“Naomba kama
inawezekana wote tuseme
Katiba Inayopendekezwa
hapana, hapana, hapana!
Badala ya kulumbana
tuangalie kesho, hatutaki
uchaguzi mkuu wa
kumwaga damu,” alisisitiza
Mbatia.
Mwanasiasa huyo
aliyetangaza nia ya
kuwania ubunge katika
Jimbo la Vunjo, aliishauri
Serikali iwakukutanishe
haraka viongozi wa vyama
vya siasa kutafuta
maridhiano ya kitaifa kwa
kuwa Ukawa hawako tayari
kuigeuza nchi kuwa ya
machafuko.
Chanzo:Mwananchi.

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top