SEKTA ya bima nchini imerahisisha huduma
za bima ya afya baada ya jana Kampuni ya
Bima ya Jubilee Insurance kuzindua huduma
ya BimaAfya ambayo watumiaji wake
wakiwemo wa kipato cha chini wataweza
kujiunga kupitia huduma ya M-Pesa ya
kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom
Tanzania.
Huduma hiyo mpya ya BimaAfya ina unafuu
mkubwa na inawalenga watu binafsi na
familia kwa ujumla ili kuwezesha
watakaojiunga kupata huduma za matibabu
ya bure katika hospitali zaidi ya 150 nchi
nzima, kuanzia wenye magonjwa ya kutibiwa
mara moja, wanaolazwa, wajawazito na
kadhalika.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano
wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,
akizungumzia huduma hiyo baada ya
kuzinduliwa jana, alisema: “Tanzania kama
zilivyo nchi nyingine za Afrika kwa muda
mrefu haina utamaduni unaowezesha
wananchi wake wote kuchangia na kufaidika
na mfumo wa bima ya afya zaidi ya
wafanyakazi ambao wameajiriwa katika
sekta rasmi.
Naye Mtendaji Mkuu wa kampuni ya huduma
za bima ya Jubilee, George Alande, alisema
takwimu zinaonesha asilimia 18 ya
Watanzania ndio wanafaidika na huduma za
bima ya afya nchini wengi wao wakiwa ni
waajiriwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni
ya Edge Point ambayo pia ina ubia katika
ushirikiano huu wa kutoa huduma ya
BimaAfya, Lilian Makoi alisema; “BimaAfya
imebuniwa kuwapunguzia mzigo wa gharama
za matibabu Watanzania wenye kipato cha
chini hususani wale waliojiajiri katika sekta
isiyo rasmi”.
posted from Bloggeroid
Post a Comment