Jamani jamani jamani!!! Hakuna siku nimesikia
uchungu kama siku hii nilipomuona huyu mtoto
aliyetelekezwa na baba yake ambae ni Mh
Mbunge... !!!!!!!!!!
kilichonihuzunisha zaidi ni pale
nilipogundua huyu mtoto ni mlemavu.... yaani
hawezi kukaa, haongei, inabidi akisiwe kama ana
njaa pamoja na vitu vingine!! kwa kifupi huyu
mtoto anahitaji uangalizi wa ziada.... yaani hata
mama hawezi kumuacha huyu mtoto nyumbani
aseme akajihangaikie apate chochote ili wale
jamani...
Yaani siku zinavyozidi kwenda kuna wimbi
kubwa sana la ''wanaume'' kutelekeza familia
zao...tatizo hili linakuwa kwa kasi kubwa mno
kiasi kwamba inabidi hata sheria maalum
itungwe kwa ajili ya kulidhibiti jamani kha!!!!!
Hawa ameieleza ''Wanawakelive kwamba
Mume wake ni Mbunge wa Dimani ambae
kipindi anagombea ubunge alipambana na
alikuwa mstari wa mbele kumsaidia kufanya
kampeni ili ashinde, lakini cha ajabu tangu
mumewe huyo apate Ubunge amekuwa
akimnyanyasa sana...
Hawa amedai kwamba amejaaliwa kuzaa
watoto watatu na huyu Mume Mheshimiwa
Mbunge! cha ajabu zaidi ni Hawa anadai
alipozaa huyu mtoto wake wa tatu ambae ni
mlemavu ndo visa viliongezeka kiasi cha kufikia
kufukuzwa ndani ya nyumba yake ambayo
walijenga pamoja na Mbunge huyo kuoa mke
mwingine....
Kinachomuuma Hawa ni kwanini Mbunge
amfukuze kwenye nyumba yake tena na mtoto
mlemavu pekee huku Mheshimiwa akibakia na
watoto wawili ambao hawana tatizo?????
Aisee kisa cha Hawa kufanyiwa unyanyasaji
huu tena na Mbunge wa jimbo! naskia kudata
maana siku hizi imekuwa kama fasheni
wanaume kuwatelekeza wake zao na watoto
bila matunzo yoyote... sasa ikiwa na KIONGOZI
atafanya unyama kama huu itakuwaje kwa
watu wa kawaida?????
Nashauri huyu Mbunge
achukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe
fundisho na kwa wazazi wengine wanaozaa na
kukimbia wajibu wao kwa familia zao.....Eti
Mheshimiwa!! nyumba yake moja imemshinda
ataongozaje jimbo lenye maelfu ya kaya!!!!
puuuuuuuuu Jamani wanawake tubadilike
katika kuchagua Viongozi... tuamke sasa
tusidanganywe na kanga na kofia ili kupiga
kura waathirika wakubwa ni sisi, mabadiliko ni
sisi jamani NGACHOKA!!
Hayo na mengine
mengi utayapata Wanawakelive, Usikose
kufuatilia kisa hichi cha kusikitisha na kuumiza
sana!!!
Credit:Joyce Kiria
Tutembelee MJUMBE BLOG kila mara mtandaoni kwa Picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu kila mara.
posted from Bloggeroid
Post a Comment