Wabunge kutoka mkoani Arusha wanatarajia
kuanzisha upya mjadala wa kutaka kufukuzwa
Bungeni na Spika Anne Makinda iwapo Prof.
Muhongo hatakuwa amewajibishwa au kujiuzulu
mwenyewe kufuatia maazimio ya Bunge
yaliyotaka Waziri huyo wa Nishati na Madini
awajibishwe kutokana na kutowajibika katika
sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow mwaka jana.
Wabunge hao ni Mbunge wa Arusha Mjini
Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru
Mashariki Joshua Nassari.
Akizungumzia na wananchi kwenye mkutano
wa hadhara Manispaa ya Moshi Lema alisema
kuwa atakuwa mbunge wa kwanza kufukuzwa
katika kikao cha Bunge kijacho endapo Prof.
Muhongo atakuwa hajawajibishwa.
Naye Joshua Nassari amesema kuwa atamuunga
mkono kutaka maazimio ya Bunge yatimizwe na
mamlaka zinazohusika.
Kikao cha Bunge cha 16 na 17 kiliazimia kwamba
wahusika wote katika sakata la Akaunti ya Tegeta
Esccrow wawajibishwe suala ambalo
halijatimizwa na mamlaka zinazohusika kwa
upande wa Serikali.
Kwa upande wa waliowajibishwa ni Waziri wa
Nyumba na maendeleo ya Makazi Prof .Anna
Tibaijuka, Mwanasheria mkuu wa serikali
alijiuzulu na kubakia Waziri wa Nishati na Madini
Prof Tibaijuka.
Viongozi wengine wa serikali ni wenyeviti wa
kamati tatu za Bunge ambao ni Victor
Mwambalaswa, William Ngeleja pamoja na
Andrew Chenge.
posted from Bloggeroid
Post a Comment