Unknown Unknown Author
Title: MABOSI WA ARSERNAL WAITIKISA DAR!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mabosi wa Arsenal watikisa Dar. *watembelea Makao makuu ya PSPF *wafanya mazungumzo na Mkurugenzi mkuu Bw Adam Mayingu Mabosi wa Mabi...

Mabosi wa Arsenal watikisa
Dar.

*watembelea Makao makuu ya PSPF
*wafanya mazungumzo na Mkurugenzi mkuu Bw
Adam Mayingu
Mabosi wa Mabingwa wa Kombe la FA wa
England, Arsenal, waliopo nchini kwa ziara ya
kikazi wameanza kutikisa, ambapo kampuni
nyingi zinataka ushirikiano na klabu hiyo.
Maofisa waliopo nchini ni pamoja na Mkurugenzi
wa Maendeleo na Ushirikiano, Sam Stone na
Meneja Maendeleo na Ushirikiano, Daniel Willey
wanatarajiwa kukutana na uongozi wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) Jumanne hii.
Tayari kampuni kubwa zaidi ya 20 zimetaka
ushirika na Arsenal, na majadiliano ya kibiashara
yanatarajiwa kuanza mara moja, kuona ni katika
maeneo gani na kwa mfumo upi watashirikiana.
Katika ziara hiyo inayoratibiwa na Imani Kajula
ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group,
benki mbalimbali zimetaka kufanya biashara na
Arsenal, lakini pia Quality Group, kampuni
inayomilikiwa na Rais wa Yanga, Yusuf Manji.
Stone amewaambia waandishi wa habari
Jumatatu hii jijini Dar es Salaam kwamba
wamejizatiti na japokuwa wamekuja kibiashara,
milango ipo wazi iwapo kuna kampuni za
michezo zinazotaka kushirikiana nao na kwamba
zinaweza kunufaika.
Ujumbe huo umetua nchini huku hali ya hewa
kisoka kwa klabu na timu ikiwa shwari, baada ya
Arsenal kuwafunga Manchester City mabao 2-0
Jumapili hii kwenye Uwanja wa Etihad
unaomilikiwa na mabingwa hao watetezi wa
England.
Mabao ya Santi Cazorla na Olivier Giroud
yakichanganywa na ulinzi mahiri wa kitimu,
vilitosha kuzikonga nyoyo za washabiki wa
Arsenal ndani na nje ya England, ambapo nchini
Tanzania pia washabiki wao walionekana
wakitamba mitaani, licha ya kwamba ilikuwa
usiku.
Stone alisema jijini Dar Jumatatu kwamba
wanaichukulia Tanzania kwa umuhimu mkubwa,
kutokana na ukubwa wake kijiografia, mvuto wa
watu wake kwenye soka na uwapo wa kampuni
kubwa na zinazoweza kushirikiana na Arsenal.
Tayari Arsenal wana uhusiano na kampuni na
taasisi nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Afrika
Kusini na Nigeria.


MJUMBE BLOG Tunapatikana Mtandaonio kwa picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu na Matukio ya hapa na pale kila siku.

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top