Pichani ni Taswira ya Darasa lenye makundi manne ya wanafunzi wa kike wakifundishwa Maada nne tofauti kwa wakati mmoja,Mwaka 1914;Vuga Usambara.
Naam;
Historia ni kumbukumbi ya shughuli na matendo ya kale ya jamii husika!
Hakika Tume piga hatua!
Tanzania Kama Taifa huru na Jamuhuri ya Muungano,Tuna historia yetu.
Katika sekta ya Elimu ya Sekondari,
>Tume ongeza Udahili wa idadi ya wanafunzi wa kike na kiume wanao jiunga kidato cha kwanza.
>Tume ongeza Idadi ya Sekondari karibia kila kata kuna sekondari moja au zaidi.
>Tume ongeza idadi ya Walimu kwenye kila shule.
>Tume ongeza idadi ya shule za watoto wa kike.
>Tume jenga Mabweni kwa ajili ya Watoto wa kike katika baadhi ya shule nchini.
>Tume Ongeza idadi ya vitabu vya kiada na rejea katika kila taasisi.
>Tume weka nishati ya umeme au Nishati Mbadala ya mwanga wa jua katika kila taasisi.
>Tume washirikisha wananchi katika ujenzi wa taasisi hizo za kielimu kwenye kila hatua na wao ndio walio kuwa washauri na waamuzi wa awali kwenye kila Hatua.
>Tume punguza mimba za utotoni kwa vijana ambao muda mwingi wa awali maishani mwao wamekuwa wakipoteza katika taasisi za Elimu.
#Changamoto kubwa katika Shule au Taasisi zetu nyingi za sekondari nchini:
>Walimu Kukosa ali ya kufundisha kutokana na kutolipwa malimbikizo ya madai yao yanayo jitokeza kila mwaka hivyo kushusha taalima katika taasisi hizo.
>Kukosekana kwa walimu wa masomo ya Sayansi katika shule nyingi za Sekondari
>Upungufu wa vyumba bora vyenye mahitaji ya msingi kwa ajili ya kufundishia!
Vingi vina jaza idadi kubwa ya wanafunzi na havina fenicha za kutosha.
>Ujenzi wa Miundombinu ya kufundishia Mibovu na yenye kiwango cha chini mno,ambayo huwa haidumu hata misimu minne.
>Kuto kuwepo na Maabara na Maktaba za uhakika kwenye kila shule/Taasisi badala yake baadhi ya shule zime geuza Madarasa kuwa Maabara.
>Kukosekana kwa vifaa vya Maabara na mahijati muhimu ya Maktaba.
>Ukosefu wa Watawala wenye Ujuzi na Upeo endelevu wa kuweza kuendana na mahitaji ya wakati,Watawala wengi hawana taaluma ya kutosha kulingana na Mahitaji ya wakati badala yake wana tumia Uzoefu tu bila Ujuzi,Weredi na Umahiri.
Wengi wame pewa dhamana kuongoza taasisi za Elimu ile hali hata wao wenyewe wana Ufahamu nusu au Hawaja jiendeleza kitaaluma.
>Uhaba wa Nyumba bora za walimu,ambapo walimu wengi hupanga mitaani ambako ni zaidi ya maili moja kutoka ilipo Shule husika! Na hata wenye vyumba wanaishi kwenye mazingira magumu mno.
Zipo changamoyo nyingi Lakini leo tuzitazame hizo kwa Uchache wake.
MJUMBE BLOG Tunapatikana Mtandaoni kwa picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu na Matukio ya hapa na pale kila siku.
posted from Bloggeroid
Post a Comment