HABARI zilizotufikia mda huu zinasema Jeshi la
Polisi Mkoani Dar es Salaam limetumia nguvu
kwa kurusha mabomu ya machozi ili
kuwatawanya wananchama cha Wananchi CUF
waliokuwa kwenye maandamo wilaya ya
Temeke .
Na kufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi
waandamizi wa chama cha Wananchi
CUF,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama
hicho Profesa Ibrahimu Lipumba,huku wananchi
wa maeneo hayo wakiishi kwa hofu kubwa sana.
Akithibitisha kukamatwa viongozi hao pamoja na
kuvunjwa kwa maandamano .Afisa Habari wa
chama cha Cuf ,Bwana Silas alipoongea na
mtandao huu mda huu ambapo amesema
waalianza maandamano ya Amani katika
Viwanja vya temeke na kwenda mbagala ,
ambapo maandamano hayo yaliokuwa na lengo
la kumbukumbu ya mauaji ya wanachama wao
yaliofanyika TAREHE 26 januari mwaka 2001
huko Zanzibari na Tanzania Bara,
Bwana Silas alisema wakati wapo kwenye
maandamo hayo walipofika maeneo ya Mtongani
iliyopo wilaya ya Temeke ndipo Jeshi la polisi
likafika na kurusha mabomu na kuwapiga
wanachama wa chama hicho na kufanikiwa
kuwakamata viongozi wa chama hicho,na
kuwapeleke kituo kikuu cha polisi.kwa madai
maandamano hayo hayana ruhusa.
ENDELEA KUFUATALIA MJUMBE BLOG UTAPATA
HABARI KAMILI NA PICHA ZAIDI ZA MATUKIO.
Post a Comment