Unknown Unknown Author
Title: MAGUFULI AZINDUA BARABARA ZA PETE!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Magufuli Azindua Ujenzi Wa Barabara Za Pete Jijini Dar es salaam Waziri wa Ujenzi Mheshimkiwa Dkt.John Pombe Magufuli leo amez...

Waziri Magufuli Azindua Ujenzi
Wa Barabara Za Pete Jijini Dar es
salaam


Waziri wa Ujenzi Mheshimkiwa Dkt.John Pombe
Magufuli leo amezindua na kuweka mawe ya
msingi katika Ujenzi wa barabara za pete
zitakazopunguza msongamano jijini Dar es
salaam.
Barabara hizo zilizowekewa mawe ya msingi ni
pamoja na ile ya Kinyerezi –Kifuru hadi Mbezi
Mwisho yenye urefu wa kilometa 14.0, Kigogo-
Tabata Dampo yenye urefu wa kilometa 1.6, na
Kimara Baruti-Msewe hadi Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam yenye urefu wa kilometa 2.6. Barabara
nyingine ni ile ya External –Kilungure hadi Kimara
Korogwe kilometa 8.0, Wazo Hill-Goba hadi Mbezi
mwisho kilometa 20 na Goba-Tangi bovu
kilometa 9.0.
Akizungumza wakati akizindua ujenzi wa
barabara hizo Waziri Magufuli amewataka
wananchi kufuata sheria za barabarani kwa
kutoingilia hifadhi za barabara na wale wenye
nyumba pembeni mwa barabara kuzibomoa
wenyewe ili kupisha ujenzi huo kwenda kwa
wakati.
“Nawahakikishieni kwamba mkifuata sheria za
kutojenga karibu na barabara barabara hizi
zitajengwa kwa kiwango cha lami na kwa wakati
ili kupunguza msongamano wa magari katika
barabara kuu na ninyi mtanufaika na fursa za
kibiashara kwa kuwa karibu na barabara za lami
na hivyo kujikwamua kiuchumi”,amesisitiza Waziri
Dkt. Magufuli.
Waziri Magufuli amesema barabara ya Wazo HilL
–Goba yenye urefu wa kilometa 20 ikikamilika
kwa kiwango cha lami itaziunganisha barabara za
Bagamoyo na Morogoro ambazo zimekuwa
zikikabiliwa na msongamano kwa muda mrefu.
Aidha, amesema barabara ya Kinyerezi- Kifuru
hadi Mbezi mwisho yenye urefu wa kilometa 14
itapunguza pia msongamano kwa kiasi kikubwa
kwa kuwa itakuwa inaunganisha barabara ya
Morogoro na Nyerere hivyo kuwataka wananchi
kuanza kuzitumia barabara hizo ambazo
zitakamilika kwa wakati.


MJUMBE BLOG ni pahali sahihi kwa wewe kujipatia Picha za matukio mbali mbali,Habari mpya,Taarifa muhimu Kila mara.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top