Nimesikitishwa sana na orodha
ndefu ya vijana wanaoshikiliwa
na wengine wameshatolewa
hukumu ya kunyogwa wengi
wao ni kutoka Tanzania, lakini
hii inatokana na vijana wengi
wa kitanzania kudanganywa
kwa kutaka utajiri wa haraka
haraka.
Usijaribu wala usidanganywe
kupeleka madawa ya kulevya
hasa katika miji ya Macao,
Hongkong,Indonesia, maana ni
hatari sana kwani kifungo cha
chini kabisa kwa gram moja ni 7
years,ila wengi uhukumiwa kwa
kunyogwa na kifungo cha
maisha na kazi ngumu.
Matajiri wengi uwadanganya
vijana matokeo yake uishia
magerezani na kunyongwa.
Jana Indonesia imewapiga risasi
raia wa nchi tano zikiwemo
zenye nguvu kiuchumi kwa raia
wake kuingiza madawa ya
kulevya nchini humo,licha ya
nchi hizo kuwaita nyumbani
mabalozi wake.
Jamani usidanganywe heti
utafungwa miaka 2 utatoka,
matajiri waelezeni ukweli kabla
ya kuwatuma huko, mimi
nilikuwa mji wa Macau ukweli
hali inasikitisha kwa watanzania
wanateseka sana.
posted from Bloggeroid
Post a Comment