MWENYEKITI wa Soko la Sowetojijini
Mbeya, Honola Mbogella,
amefikishwakatika mahakama ya Mwanzo
Mbeya mjini kwa tuhuma za kuzuia
watumishi wa umma kufanya kazi zao.
Kufuatia kukamatwa kwa Mwenyekiti
huyo kulisababisha zaidi
yawafanyabiashara 1000 wanaondesha
shughuli zao za kibiashara katika
masokomatano yaliyopo Jijini Mbeya,
kuandamana na kuizunguka mahakama ya
Mwanzo yaMbeya mjini, wakishinikiza
mahakama hiyo kumuachia huru.
Mwenyekiti huyo,amefikishwa katika
mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini,
leo na kesi yake kusikilizwa majira
ya saa tatu asubuhi ambapo kesi
hiyo ilivuta hisia za watukutokana
na kundi hilo la wafanyabiashara
kuizunguka mahakama hiyo, huku
jeshila polisi likilazimika
kuimarisha ulinzi.
Akisomewa mashitaka hayo Mbele ya
Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya
Mbeya MjiniUbaswege Mathew, karani
wa Mahakama hiyo, Sioni Kasunga,
alisema mtuhumiwa huyoalifanya kosa
hilo January 10 mwaka huu akiwa
katika eneo lake la kazi la Sokola
Soweto lililopo Jijini
Mbeya.
Alisema, kwa mujibu wa
kifungu kidogocha cha sheria namba
101(a) sura ya 288iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa
aliwazuia watumishi wa umma
wahalmashauri ya Jiji la Mbeya
kufanya kazi yao ya kukusanya
ushuru.
Alisema, mtuhumiwa
aliwazuiawafanyabiashara hao kugoma
kutozwaushuru wa shilingi 200 hadi
300 na halmashauri ya Jiji la Mbeya
kwa maelezokwamba licha ya
wafanyabiashara hao kulipiatozo hiyo
kwa kipindi kirefu bado soko hilo
limeendelea kukithiri kwa uchafu.
Aidha, kutokana na kosa hilo,Hakimu
wa mahakama hiyo, Ubaswege
Mathew,baada ya kusikiliza maelezo
hayo,alitoanafasi kwa mtuhumiwa
ambaye alikana shitaka hilo hivyo,
hakimu kuhairisha kesi hiyo mpaka
kesho na kwamba dhamana kwa
mtuhumiwa ipo wazi.
“Kesi hii nimeihairisha mpaka
kesho asubuhi, mtuhumiwa anahaki ya
kuwekewadhamana kwa masharti ya
kiasi cha fedha cha shilingi milioni
mbili na wadhaminiwawili mmoja akiwa
ni mtumishi wa
serikali,”alisema Wakati kesi hiyo
ikiendeleamahakamani hapo, umati
mkubwa wa wafanyabiashara
wanaoendesha shughuli zaokatika
masoko matano ya Soweto,Uyole,
Mabatini, Sokomatola na
Uhindiniulijitokeza na kuizunguka
mahakama hiyo kwa kile walichokidai
kwamba Mwenyekityi huyo ameonewa.
Wakizungumza naMbeya yetu ,nje ya
mahakama, wafanyabiashara hao ambao
waligoma kutaja majina yao,
walisemawao wamegoma kulipa ushuru
huo kutokana na halmashauri
kushindwa kuetekelezamajukumu yao ya
ukarabati wa miundombinu pamoja na
usafi wa mazingira hivyoMwenyekiti
huyo hausiki na suala
lakuwashawishi kugoma kama
inavyodaiwa na halmashauri.
Hata hivyo, wafanyabiashara
haowamegoma kuendelea na shughuli
zao mpaka suala hilo litakapo patiwa
ufumbuzikwa halmashauri kurekebisha
miundombinu na usafi wa mazingira
katika maeneo yabiashara.
Mwisho.
Picha zaidi
Tembelea MJUMBE BLOG Mtandaoni Kwa Picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu,Matangazo na Matukio kila mara.
Post a Comment