Waziri wa Usalama nchini Kenya, Joseph Nkaissery
amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi
ya Lang’ata baada ya kupigwa mabomu ya
machozi na Polisi juzi walipoandamana kupinga
kunyang’anywa kipande cha ardhi ambacho
kilikuwa uwanja wao wa kuchezea ana baadae
kuuzwa kwa mtu na kuwekewa uzio. Na inaelezwa
pia aliyaamuru mabomu kupigwa amefutwa kazi.
Rais Uhuru Kenyatta amelaani tukio hilo na
kumtaka Waziri wa Ardhi, Charity Ngilu na
Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi, Mohammed
Swazuri kuwajibika na kueleza kwanini walizembea,
huku Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo pia kalaumiwa
kwa kushindwa kuzuia watoto hao kujihusisha na
vurugu.
posted from Bloggeroid
Post a Comment