Unknown Unknown Author
Title: WALIMU MBEYA WALIPO ANDAMANA KUDAI HAKI ZAO;WAMWOMBA RWEGAMALILA AWASAIDIE!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Walimu wakiwa wamezuiwa na FFU wasiendelee na maandamana. WALIMU wa shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, ...



Walimu wakiwa wamezuiwa na FFU wasiendelee na maandamana.

WALIMU wa shule za Msingi na Sekondari katika
Halmashauri ya Jiji la Mbeya, wapatao 113, juzi
waliandamana kuelekea ofisi ya Mkurugenzi wa
Jiji hilo kwa ajili ya kudai haki zao mbalimbali.
Maandamano hayo ya amani, yalianzia katika
ofisi kuu ya Jengo la CWT Mkoa wa Mbeya majira
ya saa 5;27 asubuhi, kabla hayajazuiwa na kikosi
cha askari wa kutuliza ghasia mkoani hapa saa
5;33 mpaka saa 5;39 na kuwaomba warejee
ofisini kwao kutokana na hali ya vurugu iliyokuwa
imelizingira Jiji hilo jana.
“Tunawaomba mrudi ofisini kwenu na sisi
tutaenda kumleta Mkurugenzi wa Jiji, kwasababu
hata mkijaribu kwenda muda huu hamtaweza
kuonana naye, ulinzi umeimarishwa sana
kutokana na mgomo wa wafanyabiashara wa
soko la Soweto ambao wamegoma na wanataka
kuandamana” alisikika mmoja wa askari mwenye
nyota tatu, akiwasihi walimu hao.
Wakizungumza na waandishi wa habari, walimu
hao walisema kuwa, walifikia uamuzi wa kwenda
kumuona mwajiri wao kutokana na madai
mbalimbali yakiwemo malimbikizo ya mishahara
yao tangu mwaka 2007.
“Mwalimu unaingia darasani ukiwa na mawazo ya
fedha zako huku ukiangalia dawati la mwanafunzi
limechoka. Serikali inajisikia raha kuona mwalimu
anaenda na biashara ya ubuyu shuleni! Mimi
nadai zaidi ya Milioni Nne tangu mwaka 2007
sijalipwa na fedha tunaambiwa zimekuja
zinafanya kazi zingine”alisema Mwalimu Stella
Robson.
Mwalimu Lucas Mahenge, ambaye ni mlemavu wa
macho, alisema kuwa yeye madai yake ni suala la
kupandishwa madaraja bila kupandishwa
mshahara, hali ambayo alisema inamkatisha
tamaa na serikali isifikie mahala ikawafikirisha
walimu kuanza kuwafundisha watoto kuwa
2+2=22.
“Serikali kama imeshindwa kutulipa madai yetu,
ituambie ili tuweze kumwomba mfanyabiashara,
Rwegemalil” alisema Mwalimu Gunza
Mwasomola.
Katibu wa Chama cha walimu Jiji la Mbeya,
Mwalimu Felix Mnyanyi, alisema kuwa kwa
kushirikiana na viongozi wenzake, wamefuatilia
kwa muda mrefu madai hayo na kufanya uhakiki
lakini utekelezaji wake umekuwa siyo wa
kuridhisha.
“Walimu wamefika hapa wakiwa na madai zaidi
ya matatu, ambayo ni malimbikizo ya mishahara
tangu mwaka 2007, ambapo ni wilaya pekee
nchini walimu hawajalipwa, madai ya fedha za
likizo, kupanda na kushushwa madaraja baada ya
kujiendeleza kitaaluma na walimu wastaafu
kutolipwa” alisema Mwalimu Mnyanyi.
Alisema kuwa baada ya kuzuiwa na kuwaelewa
askari polisi kuwa wasifike katika ofisi ya mwajiri
wao ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya,
kutokana na hali ilivyokuwa ya utata wa usalama
wao na watu wengine, walirejea ofisini hapo na
kuendelea kumsubiri mwajiri huyo chini ya ulinzi
wa polisi, hali ambayo mpaka majira ya saa saba
mchana, walimu waliendelea kuwepo katika ofisi
yao na Mkurugenzi hakuweza kufika kwa wakati
huo mpaka tunaenda mitamboni.
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Mussa Zungiza,
alikiri kuwepo madai ya walimu katika ofisi yake
na kwamba madeni hayo hayatawezwa
kumalizwa kwa siku moja kutokana na walimu
kutofautiana muda wa kuanza likizo na kumaliza.
Alwaambia walimu kuwa atashughulikia madai
yao kwa kushirikiana na uongozi wao wa CWT.
(Tunaenda)...

Tumbelee MJUMBE BLOG Mtandaoni upate Picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu kila mara.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top