Unknown Unknown Author
Title: WANAWAKE WENYE MAPAJA NA MAKALIO MAKUBWA NI DILI ZAIDI:ETI MAFUTA YA MWILI HUKUZA UBONGO?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Makalio ya mwanamitindo na mlimbwende Kim Kardashian yamekuwa gumzo kubwa duniani kote Fumbo la siku zote kwamba wanawake ni wanene ku...

Makalio ya mwanamitindo na mlimbwende Kim
Kardashian yamekuwa gumzo kubwa duniani kote


Fumbo la siku zote kwamba wanawake ni
wanene kuliko wanaume limepata ufumbuzi...ni
wanene kwa wanahitaji mwili wenye umbo zuri
na makalio makubwa ili kupata watoto
waliojaaliwa werevu.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa wanaakademia
ambao wanasema kuwa wanawake wenye
makalio na mapaja makubwa na umbo zuri
kutokana na mafuta mfano kama Kim Kardashian
hupata watoto werevu.
Nini hasa kinawafanya watoto wao kuwa werevu
basi?
Mafuta yanayopatikana katika sehemu za
mwili wa mwanamke huwa na manufaa makubwa
sana kwa watoto hasa wanapokuwa wananyonya,
mafuta haya hupitia kwenye maziwa ya mama
hadi kwa mwili wa mtoto.
Profesa Will Lassek wa chuo kikuu cha Pittsburgh
University, Pennsylvania, aliyeongoza utafiti huo,
anasema mafuta yanayopatikana katika sehemu
hizo za mwili, husaidia sana katika kukuza
ubongo wa matoto mchanga.


Ubongo wa binadamu
'Unahitaji mafuta mengi ya mwilini ili kuwa na
mfumo mzuri wa neva na mafuta katika sehemu
hizi za mwili yaani mapaja na makalio, huwa yina
madini yajulikanayo kama DHA (docosahexaenoic
acid), ambayo ni muhimu sana katika kutengeza
ubongo wa binadamu.
Inaonekana kama wanawake wameweza kujua
mbinu za kuhifadhi mafuta katika sehemu hizo za
mwili hadi wanapopata mtoto.


Kwa mda mrefu haijajulikana kwa nini wanawake
wanakuwa wanene sana.......mafuta ya mwili
wao yakiwa ni asilimia 30 ya uzani wa mwili.
Professa Lassek anasema kwamba mafuta hayo
ni kiwango sawa na yale yanayopatikana katika
wanyama kama Dubu au Nyangumi
wanapojiandaa kuzaa.
Wanasayansi wanasema mafuta yanayopatikana
katika mapaja na makalio ya wanawake ndio
yanayotumika kutengeza ubongo wa watoto
wachanga.


Mafuta mengi katika mwili wa mwanamke huisha
mwilini pindi mama anapomnyonyesha mtoto
wake, kulingana na Profesa Lassek, aliyechapisha
utafiti wake katika kitabu chake kipya chenye
kichwa ''Kwa nini wanawake wanahitaji mafuta
mwilini. ''

Wanawake wanaonyonyesha hupoteza kilo nusu
ya mafuta mwilini kila mwezi.
Chanzo:bbc


Tutembelee MJUMBE BLOG Mtandaoni Kila mara upate Matukio pichani,Habari mpya,Taarifa muhimu,Matangazo kila mara.

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top