Zacaria aliyeibuka na madai mapya.
Mfungwa Zacarias Moussaoui, aliyefungwa
katika gereza la Colorado ,ambaye picha yake
haikuwahi kuoneshwa, ameibuka na madai
mapya .
Zacarias Moussaoui ameshatumikia kifungo cha
muda wa miaka nane gerezani,Zac ni
mwanachama wa kundi la Al-Qaeda ambaye kazi
yake kubwa ilikuwa ni ulipuaji majengo na hivi
karibuni amedai kuwa baadhi ya wana familia ya
kifalme ya Saudi Arabia walisaidia ufadhili wa
shambulio la Septemba kumia na moja .
Saudi Arabia tayari imekanusha madai hayo
yaliyotolewa na mhalifu huyo na kudai kuwa
hayana maana.
Katika mahojiano ya kipekee na mfungwa huyo
yaliyofanywa kwenye gereza lililo chini ya ulinzi
mkali,Zac amewataja maofisa wa serikali ya
Saudi Arabia akiwemo mwana wa mfalme al-
Faisal Al Saud,ambaye aliwahi kuwa mkuu wa
usalama ambaye anadaiwa kulifadhili kundi hilo la
Al-Qaed mwishoni mwa mwaka 1990.
Madai yake hayakuishia hapo, amedai pia kuwa
alishawahi kukutana na maofisa wa juu wan chi
hiyo huko Afghanistan na kuzungumza na ofisa
wa ubalozi wa Marekani nchini humo .
Shambulio la September kumi na moja liligharimu
maisha ya watu karibu elfu tatu .
Zac na ofisa huyo wa ubalozi pamoja walitarajiwa
kusafiri hadi mjini Washington kutafuta eneo zuri
la la kuweka kombora la mashambulizi ambayo
kama yangefanikiwa wangeidungua ndege ya air
Force One,madai hayo .Zac anadai kuwa
aliyafanya chini ya kiapo kikali na hayakuwahi
kutambulika.
Moussaoui alikamatwa wiki kadhaa kabla ya
utekelezaji wa shambulio la September kumi na
moja ,na alikamatwa kwa madai ya kutokidhi
vigezo vya uhamiaji na wakati huo wa shambulizi
la kigaidi yeye alikuwa jela tayari .Zac alipewa
mafunzo ya urubani huko Minnesota na amekuwa
akijihusisha na usambazaji pesa kwa mtandao
zinazohusiana na kundi hilo la Al qaeda .
Mpango mwingine wa Moussaoui ilikuwa
kutekeleza kazi aliyopangiwa ya kurusha ndege
aina ya 747 na kuielekeza Ikulu ya Marekani .
chanzo:
MJUMBE BLOG Tunashukuru kwa kututembelea.
Post a Comment