Wimbi la vituo vya Polisi kuvamiwa na kuporwa
silaha linazidi kushamili kufuatia kituo kingine cha
Polisi cha Mngeta Kilombero mkoani Morogoro
kuvamiwa na kundi la Majambazi na kuporwa
bunduki aina ya SMG yenye risasi 30.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Morogoro, Leonard Paul alisema uporaji huo
ulitokea usiku wa Februari Mosi ambapo licha ya
kupora silaha waliiba pia jenereta, redio, viti, berti
ya Gari pamoja na spika ya redio.
Hadi sasa kituo hicho ni cha tatu kuvamiwa
ambapo vituo vingine ni Kituo Kikuu cha Polisi
Rufiji, Mkoa wa Pwani na Bukombe kuvamiwa na
majambazi na kuua polisi wawili na kupora
bunduki saba na risasi 60. Mwaka jana
majambazi walivamia Kituo cha Polisi Mkamba,
wilayani Mkuranga, Pwani na kuua askari mmoja
na mgambo wawili kisha kupora bunduki tano na
risasi 60, pamoja na tukio la Polisi kuporwa silaha
mkoani Tanga.
Kwa upande mwingine Kamanda Paulo alisema
baada ya wizi huo askari walianza msako na
kufanikiwa kuipata bunduki hiyo na risasi 30, viti
vitatu, jenereta na redio vikiwa vimefichwa katika
pori la Simbangingile lililopo Mngeta Wilaya ya
Kilombero.
Jeshi la Polisi inawashikilia watu watatu kutokana
na tukio hilo ambao ni Ramadhani Shewele (20),
Hamisi Ahmed (45) na Ignus Shewele (34) wote
wakazi wa Nakagulu.
MJUMBE BLOG Tuna shukuru kwa kututembelea
Post a Comment