MIKOA sita ‘imevurunda’ katika ujenzi wa
maabara katika shule za sekondari baada
ya kushindwa kufikia malengo. Ni mikoa
mitatu pekee ndiyo imefanya vizuri kwa
kuvuka nusu ya malengo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alitaja mikoa
ambayo haikufika hata robo ya malengo
kuwa ni
Mtwara (asilimia 21),
Lindi(asilimia 20),
Tabora (asilimia 17),
Dodoma (asilimia 12),
Rukwa (asilimia
11) na
Kigoma (asilimia 10).
“Tunaweza kusema hii ndiyo mikoa ya
mwisho katika kutekeleza agizo la Rais.
Mikoa 16 ambayo sikuitaja hapa iko
katika kundi la asilimia kati ya 26 hadi
49,”
alisema Pinda jana kupitia hotuba
yake ya kuahirisha Bunge la 18.
Pinda alitaja mikoa mitatu iliyofanya vizuri
kuwa ni
Njombe uliofanikiwa kukamilisha
ujenzi kwa asilimia 96 wa maabara za
shule za sekondari,
Ruvuma iliyokamilisha
kwa asilimia 81
na Morogoro ambao ni
watatu kwa kujenga vyumba kwa asilimia
53.
Waziri Mkuu alipongeza Ruvuma na
Njombe kwa kutekeleza vizuri maelekezo
ya Rais, akisema imeonesha mfano mzuri.
Alisema Morogoro ni wa tatu. Alisema
Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake
kwa wananchi, Desemba 31 mwaka jana,
aliongeza miezi sita zaidi hadi Juni 2015
kwa ambao hawajakamilisha ujenzi wa
maabara hizo, ili wakamilishe.
Pinda alisema matarajio ya Rais Kikwete
ni kwamba muda huo unatosha kwa kila
sekondari nchini kuwa na vyumba vitatu
vya maabara .
“Hivyo, ninawataka wakuu
wa mikoa, wakuu wa wilaya, mameya,
wenyeviti na wakurugenzi watendaji wa
halmashauri za wilaya na miji nchini
kuhakikisha maagizo haya yanatekelezwa.
Aidha, ninatoa rai kwa waheshimiwa
wabunge na madiwani kutoa msukumo
stahiki katika utekelezaji wa maagizo haya
kwa maslahi ya Taifa letu,” alisema. Kwa
upande wa Serikali, Pinda alisema Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (Tamisemi), haina budi
kuhakikisha agizo linatekelezwa ndani ya
muda uliotolewa; yaani Juni mwaka huu.
Aidha, alisisitiza katika usimamizi,
Tamisemi ihakikishe vyumba vya maabara
vinavyojengwa vinakuwa na ubora stahiki
na vinalingana na thamani ya fedha
zilizotumika.
Amesema ubadhirifu wa aina yoyote
usipewe nafasi na watakaobainika
kuhusika wachukuliwe hatua za kisheria
mapema.
“Nitapenda Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tamisemi waendelee kufuatilia
suala hili na kunipa taarifa mara kwa
mara,” alisema.
Mwaka 2012, Rais Kikwete akiwa ziarani
katika mkoa wa Singida, alielekeza kila
shule ya sekondari nchini iwe ina vyumba
vitatu vya maabara ifikapo Novemba 30,
2014.
MJUMBE BLOG
Tunakupongeza kwa kuamua kutumia huduma zetu.
HONGERA.
Post a Comment