SERIKALI imesema Tume ya Utumishi wa
Walimu itaanza kazi Julai mwaka huu na
kuhudumia walimu katika masuala
mbalimbali huku muundo wa utumishi wa
tume hiyo umehusisha ngazi za chini na
juu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani
alisema serikali imekubali kuanzisha tume
hiyo ya kuhudumia walimu nchini ili
kuepuka walimu kuhudumiwa na wizara
mbalimbali.
Alisema tume hiyo itaanza rasmi mwezi
huo na kuingizwa kwenye bajeti ijayo,
huku madeni ya walimu ya mishahara
yakiwa ni yaliyohakikiwa Sh bilioni sita na
ambayo hayajahakikiwa ni Sh bilioni tatu.
Alisema ili kukabiliana na madeni ya
walimu, sasa serikali imeagiza taasisi zote
ziweke kipaumbele katika malipo ya likizo
iwe kulipwa mapema kama mishahara.
Awali, Kamati ya Huduma za Jamii ilitaka
walimu nchini kusajiliwa ikiwa ni pamoja
na wanaofanya kazi katika shule binafsi ili
kuwatambua walimu na kuweka kiwango
cha msingi cha kutoa huduma kwa walimu
nchini kwa kuitumia Tume ya Utumishi
wa Walimu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Margaret
Sitta alisema kamati inapongeza kusudio
la serikali kuanzisha Tume ya Utumishi
wa Walimu nchini katika mwaka wa fedha
2015/16.
Alisema kamati inashauri tume hiyo
kuanzishwa haraka ili kukabiliana na adha
zinazowakabili walimu nchini na kurejesha
hadhi ya taaluma ya ualimu nchini.
MJUMBE BLOG
Tuna shukuru kwa kututembea.
Post a Comment