Unknown Unknown Author
Title: MARUFUKU KUWA FUKUZA,KUWA KARIRISHA AU KUWA STISHIA MASOMO WANAO SHINDWA KUFIKIA WAATANI! SERIKARI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Serikali imezipiga marufuku kitendo cha shule binafsi nchini kuwafukuza ama kuwasitishia masomo wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani n...

Serikali imezipiga marufuku kitendo cha shule
binafsi nchini kuwafukuza ama kuwasitishia
masomo wanafunzi wanaoshindwa kufikia
wastani na kwamba shule zote zitakazokiuka
agizo hilo zitachukuliwa hatua kali ikiwa ni
pamoja na kufutiwa usajili huku ikiongeza kuwa
kuanzia mwaka 2016 itaanza kutoa elimu bure
kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne.

Onyo hilo la serikali kwa wamiliki wa shule
binafsi za serikali limetolewa na waziri wa elimu
na mafunzo ya ufundi bungeni mjini Dodoma
katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 18
ulianza Dodoma katika kipindi cha maswali na
majibu kutokana na swali la msingi la Mh
Conchesta Rwamlaza ambapo waziri huyo
amesema ni marufuku kwa mameneja na
wamiliki wa shule binafsi za sekondari
kukaririsha, kuhamisha ama kuwafukuza shule
wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani wa
shule husika kwa kuwa kiwango cha ufaulu
kilichowekwa na serikali ni wastani wa asilimia
30.

Aidha mbunge wa handeni Dr Henry Shekifu
ameitaka serikali kutoa tamko la lini itaanza
kutoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi
kidato cha nne ili kuwawezesha watoto wote wa
Tanzania kupata elimu ambapo serikali imesema
utekelezaji wake utaanza mwakani.

Awali kabla ya kuanza kwa shughuli za bunge
spika wa bunge hilo Mh Anne Makinda
amemwapisha mwanasheria mkuu mpya wa
serikali ndugu George Mcheche Masaju.
Mara baada ya kuapishwa nje ya bunge akijibu
swali la waandishi wa habari kuhusu mswaada
wa sheria ya mahakama ya kadhi ambao
umeanza kuibua mawazo kinzani kwa baadhi ya
viongozi wa dini hasa wa kikristo ndugu Masaju
amesema wamepitia kwa umakini mswaada huo
na kwamba hauna athari zozote kwa mtu,
vikundi vya dini na taifa kwa ujumla na
hautaingilia mambo yanaayosimamiwa na
serikali ikiwemo makosa ya jinai na taifa
litaendeleaa kuwa wamoja.


MJUMBE BLOG kwa picha,Matangazo,Habari Muhimu,Taarifa mpya na Matukio yaliyo jiri kutoka kila Pandw.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top