Unknown Unknown Author
Title: MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA CCM:KIKWETE AHIMIZA KUJIANSIKISHA UPYA! ASEMA CCM ISIPO SHINDA,NCHI ITAYUMBA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
- Na sasa, M/kiti anajongea kuanza kutoa hotuba (anashangiliwa sana). JK: Mheshimiwa Makamu m/kiti wa CCM Philip Mangula, M/kiti wa NRM....

- Na sasa, M/kiti anajongea kuanza kutoa
hotuba (anashangiliwa sana).
JK: Mheshimiwa Makamu m/kiti wa CCM Philip
Mangula, M/kiti wa NRM. Huyu ni rafiki yangu
mkubwa, ni rubani pia. Alishawahi kunisafirisha
na ndege akiwa kama rubani.
- Sasa anashukuru wahusika wote na
waheshimiwa mbalimbali .
- Anammwagia sifa Mhe. Nchimbi kwa
maandalizi mazuri na kuwashukuru viongozi
mbalimbali wa CCM kwa kazi nzuri, akiwemo
Katibu mkuu, AbdulRahman Kinana.
JK: Nchi yetu imepiga hatua, kuna amani,
utulivu na maendeleo yanayoonekana. CCM
imeendelea kuaminiwa katika awamu zote. Hata
mwaka huu itakuwa hivyo hivyo. Nalisema hil
bila wasiwasi kabisa, roho baridiiiii.
Dalili ya mvua ni mawingu, ushindi tulioupata
kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Oktoba
2014 ni ushahidi tosha, ndugu zetu wapinzani
hawana chao.
Tusikate tamaa, tunaweza kuwa na changamoto
nyingi mwaka huu, ila tunapaswa kuwa na ari
zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Lazima
tuhakikishe tuwe wamoja. Umoja ni ushindi.
- Anaendelea..
JK: Komba nakushukuru sana kwa wimbo
mzuri, huishiwi nyimbo (vichekooo).
Huu ni mwaka ambao tunapaswa kuwa na
rasilimali za kutosha kuweza kuwapatia ushindi
wagombea wetu, ni mwaka wa kuhakikisha
tunafanikisha kwa kiwango kikubwa.
Nafurahishwa na wale waliofanya kazi kubwa.
Nawapongeza sana!
Nasikitishwa na viongozi wetu ambao
hawajafanya kazi ipasavyo, hawa wanavunja
moyo, wanazorotesha chama chetu. Kuna
msemo unasema ''Jasho jingi wakati wa amani,
damu kidogo wakati wa vita''.
Maana yake maandalizi yakiwa ya kutosha, kazi
inakuwa rahisi, kinyume chake unapunguza
nguvu ya ushindi. Naomba kila mmoja ajipime
yupo fungu gani.
JK: Kila wilaya na mkoa kiwe na mfuko wa
uchaguzi, na wakati ndio huu mfuko unatakiwa
kufanya kazi. Sina budi kuwatahadharisha,
msichukue fedha ambazo zitaleta matatizo!
JK: Lazima tujiandae kama chama na kuwa na
nyenzo zote kwa ajili ya kukiwezesha chama na
wagombea wetu kushinda.
Katika jitihada za kutafuta pesa za kutunisha
mifuko ya uchaguzi, Msichukue tu kila pesa,
nyingine moto. Mi ushauri wangu ni huo tu!
Huu ni mwaka wa kutambua ahadi, zipi
zimetimizwa na zipi bado. zipo ahadi za rais na
za chama kuanzia mkoa, wilaya na kata.
Mwaka wa kuulizwa ndio huu!
Waswahili husema, ''mla kunde husahau, mtupa
maganda hasahau''. Kwahiyo watupiwa
maganda hawajasahau. Lazima tuwe makini.
JK: Sio tukiulizwa, tuanze kuwanyooshea vidole
na ni kuwaita wapinzani. Kwahiyo nasisitiza kila
mmoja akumbuke ahadi zake. Mimi
nayakumbuka maana naandika, na wasaidizi
wangu hunisaidia kunikumbusha, ila kusema
kweli mengi tumetekeleza sana. Japo yapo
machache bado.
Huu ni mwaka wa kuulizwa, si vizuri tuumalize
mwaka huu huku tunaenda na madeni lukuki ya
ahadi. Kushinda tutashinda, ila yatatupunguzia.
Huu ni mwaka wa kuongeza jeshi letu la
ushindi, nalo ni wanachama wapya.
JK: Jambo lingine kubwa na la muhimu ni
kuwatembelea wanachama na wananchi
kuzungumza nao. Jambo hili huwa hatulifanyi
vizuri sana. Kila nikipata taarifa, nna watu
wengi wa kunipa taarifa, wengine hamuwajui
nawajua mie.
Wananiambia, 'Chama chako hakifanyi mikutano
mingi kama wapinzani'. Japo ukiwauliza
watajitetea. Ndugu zangu, hili ni jambo kubwa,
huwezi kupata ushindi kwa watu wasio kujua.
JK: Tuache kukaa ofisini, tutoke tuwashawishi
watu wajiunge na ccm. Kila ofisi ya mkoa na
wilaya inayo gari. La kuwawezesha kufanya kazi
hiyo lakini hamtembei. Tulipokuwa hatujawapa
magari, ajenda ilikuwa ni magari. Mpaka mzee
Mkapa akawa anakasirika. Sasa tumewapa
hayatumiwi inavyotakiwa.
Jambo la msingi ni kuwapata wapiga kura ili
tushinde. Chama chetu kama vilivyo vyama
vingine kinapaswa kuhimiza wananchi
wajitokeze kwa wingi kujitokeza kupiga kura.
Asiyekuwa na kadi mpya ya kupiga kura,
hatoruhusiwa kupiga kura, unaanza utaratibu
mpya wa BVR, kadi za zamani hazitotumika.
Tume ikitangaza, nenda, usije ukasema unacho
chako, we nenda kwa kuwa hicho cha zamani
hakitotumika.
Asiyejiandikisha hatopata fursa ya kupiga kura
ya maoni na ya uchaguzi mkuu. Hakuna
kujiandikisha tena, hii ndio ya mwisho!
Asiyejiandikisha kala hasara.
Nawasihi wanachama wetu ambao ni zaidi ya
milioni 8 wajiandikishe, ikiwa wote hawa
watajiandikisha na kupiga kura, tutapata ushindi
kwa kishindo!
JK: Ndugu wananchi, tunajua jambo kubwa ni
kura ya maoni ya Katiba pendekezwa ya hapo
machi, uandikishaji wa kupiga kura ndio lipo
mbioni. Lingine ni uchapishaji na usambazaji wa
katiba pendekezwa ili wananchi waisome.
Tuwasaidie wananchi kuwapatia elimu kuhusu
katiba inayopendekezwa na kuhamasisha
wananchi wapige kura ya ndio. Wenzetu
watatoa elimu hasi, sisi tutoe chanya. Wao
watahimiza isipite, sisi tuhimize ipite..
JK: Katiba iliyopendekezwa imebeba maslahi
mapana ya nchi yetu, nadiriki kusema hakuna
katiba bora kama hii ya sasa. Inatambua
maslahi ya makundi maalum na namna ya
kuyatimiza. Wakulima, wafugaji, wasanii,
wanawake na mengine mengi.
Katiba imeshughulikia kero za muungani vizuri.
Yale mambo yaliyokuwa yanaukwaza
muungano, yamepatiwa suluhisho. Sioni sababu
ya kukataa katiba inayopendekezwa.
Niwakumbushe, tukiikataa hii, maana yake
iliyopo itaendelea kutumika, maana hakuna
nyingine. Na itakuja kuchukua miaka mingi
ijayo. Labda rais ajaye apate hamu. Maana
mimi nilipata hamu!
Wapinzani wamesikika wakisema hawatoshiriki
na kuwataka wananchi wasishiriki. Hii
imenisikitisha. Mimi nawasishi washiriki, na
nawasihi wananchi washiriki, wao wakitaka
kususia wasusie, ila nyie pigeni kura.
JK: Nawasihi, msiache kupiga kura eti kisa tu
serikali 3 haimo, maana hawana hoja nyingine.
Sasa hivi bado hawa watu hawana muamko
nalo, ila muda ukifika muamko utakuja. Serikali
tatu haina muhemko kwa sasa.
Lakini jambo ni moja tu, kama kweli wananchi
wanataka serikali tatu, na humu haimo,
itathibitika kwenye kura. Wasiposhiriki
tutashiriki sisi na tutashinda.
Msibabaishwe na wala msirudishwe nyuma.
JK: Wananchi, Mwezi Oktoba tutafanya
uchaguzi mkuu. Utakuwa wa kihistoria kwani
tunachagua Rais wa awamu ya tano. Mimi
mwakani nitakuwa nafanya 'handover' tu, lakini
pembeni yangu atakaa MKUU WA NCHI. Mimi
nataka rais ajae awe ni wa CCM.
Maelezo ni rais, Namnukuu Mwalimu aliwahi
kusema, 'Rais wa nchi yetu anaweza kutoka
chama chochote, lakini rais bora atatoka CCM'.
Tuuenzi wosia huu mzuri.
JK: Mgombea ambaye wananchi wakisikia jina
lake tutakapomtangaza katika ukumbi wetu,
wananchi watanzania waseme, 'hapo barabara'.
JK: Kushinda chaguzi za dola, ndiyo
madhumuni makuu ya chama cha mapinduzi.
Tusipoipigia CCM, tutakuwa tumemuangusha
muasisi wetu. Aliwahi kusema bila CCM imara,
nchi itayumba. Tuhakikishe tusifanye vitendo
vitakavyokiuka, laana na hasara kwa taifa ni
kubwa, na ni msiba mkubwa kwa CCM na nchi
itayumba! Lazima tuhakikishe hatufiki huko.
Watu wazuri wapo CCM wa kutosha, naamini
mnawajua.
Mnaowaona wanafaa, washawishini wachukue
fomu, sio dhambi, hata mimi nilishawishiwa.
Ngoja nitoe siri moja, japo sio nyeti. Kinana
aliniulizaga kipindi hicho 'umemuona mzee
fulani'? Nikamjibu 'sijamwona', akaniambia
''uwe umemwona au hujamwona, we zingatia''.
Kwahiyo, Sio dhambi, mnayemuona anafaa,
mpendekezeni, hata kama anasita sita na
kusema hajajiandaa kisaikolojia, mwambieni
'wewe ndie unayetufaa'.
Nina imani tunao watu wazuri sana ambao
watatuvusha (Makofiii).
Msanii wetu Diamond yuko hapa, atatumbuiza,
ni msanii bora Afrika nzima na dunia,
anapendwa sana. Ile nyimbo yake ya My
Number One ikipigwa ile, hata mimi nishawahi
kuiimba kidogo. (Vicheko).
JK: Nikizungumzia kwa Mkoa wa Ruvuma, hali
si mbaya sana. Maana kwa takwimu za ushindi
wa kura za serikali za mtaa mwaka huu, ni
ushindi mzito. Tuimarishe zaidi. Kuhusu
maendeleo yaa Ruvuma, yanaridhisha japo kasi
zaidi inahitajika.
Kwa ufupi, Ruvuma ya miaka 10 iliyopita, si
sawa na ya leo. Mwenye macho haambiwi
tazama.
JK: Jambo la mwisho nitazungumzia kuhusu
mazao ya wakulima. Niliwahi kuelezea
kutofurahishwa kwangu na deni lisilolipwa.
Nimeagiza walipwe kwanza wakulima wale
wadogo, nasikia wanatangulia kulipwa
mawakala halafu wakulima wanacheleweshewa.
Hili liangaliwe, na walipwe kwanza wakulima
wadogo.
Hivi karibuni tutapata pesa nyingi, bilioni 36,
waziri mkuu anasema bilioni zaidi ya 10
zishaletwa, zipo, tutawapa. Safari hii
Hatutopenda kusikia tena malalamiko.
Sasa hebu tuanze safari, wizara ya kilimo na na
wizara ya viwanda na biashara washirikiane na
mikoa ya kilimo kama hii.
Namalizia, Mafanikio ya kuongoza miaka 38
isitufanye tubweteke. Tuzidi kuongoza juhudi.
Tuwe tayari kubadilika na kwenda na wakati.
Itawezekana ikiwa tutaendelea kukuza
demokrasia ndani ya chama. Na tukoseane bila
chuki ndani ya chama.
Hatuna budi kuondoa utegemezi wa kifedha,
kutegemea misaada, na hata ruzuku na
michango ya wafanyabiashara. Ipo siku watoa
misaada, na wafanyabiashara watapungua.
Tuwekeza nguvu zaidi kwenye kuzalisha kwa
kutumia vizuri rasilimali zetu, lazima tuwe
wabunifu. Hii yote ni ili kuwezesha chama chetu
kijitegemee.
Nihitimishe kwa kusema leo ni siku ya furaha
kwetu wote. Tuwakumbuke waasis japo wawili,
Mwalimu Julius K. Nyerere na Aboud Jumbe,
kwani kwa busara zao, wao ndio walioanzisha
chama cha CCM.
Kidumu chama cha mapinduzi.
- M/kiti wa CCM Taifa, ndugu JK Kikwete
ameshamaliza kutoa hotuba yake. Na sasa
ratiba nyingine za sherehe zinaendelea.
MC: Kabla m/kiti hajaondoka, nimpandishe
msanii Diamond.
JK: Mi bado nipo (vicheko)
MC: Hahaha, naona mheshimiwa bado yupo
nasi.
- Hotuba ya rais imeisha, na Msanii Diamond
anatoa burudani sasa.. (Anashangiliwa sana).
Credit:Jf

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top