Unknown Unknown Author
Title: MGABE:AFRIKA NI KWA AJILI YA WA AFRIKA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aingia madarakani kama rais mpya wa Umoja wa Afrika wa awamu ya mwaka 2015 Rais Mugabe aliyepokewa na Mwe...

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aingia
madarakani kama rais mpya wa Umoja wa Afrika
wa awamu ya mwaka 2015
Rais Mugabe aliyepokewa na Mwenyekiti wa
Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-
Zuma katika makao makuu nchini Ethiopia,
alizuru vitengo mbalimbali vya tume hiyo kwa
lengo la kutambulishana na wafanyakazi.
Mugabe aliyetoa hotuba kwa wafanyakazi wa AU
katika ukumbi wa Nelson Mandela alisema,
‘’Tume ya AU inapaswa kuwa tayari kufanya kazi
kwa ajili ya bara la Afrika. AU inapaswa kuwa na
nguvu zaidi kuliko zamani na ni lazima kuonyesha
uwezo wake wa kuondoa ufisadi, ujahili na
kuongeza idadi ya wasomi.’’
Akitoa wito wa kuongeza juhudi za kuimarisha
umoja wa muungano wa Afrika na kuetekeleza
mipango inayolenga kufikia malengo ya AU,
Mugabe alisema hivi: ‘’Tunapaswa kutambua hili:
Afrika ni bara la Waafrika. Serikali za Afrika
zinapaswa kufahamu vyanzo vinavyowafaidisha
wananchi wake. Na ili tuweze kutekeleza haya
yote, tunatakiwa kujiamini na kuweza kutoa
wasomi na wataalamu watakaosaidia kukuza
vyanzo na raslimali zenye utajiri wa Afrika.’’
Mugabe pia alisema, ‘’Tutasonga mbele daima,
na hatutarudi nyuma kamwe.’’
Mwenyekiti wa Tume ya AU Zuma naye alisema,
‘’Wakati huu ni mwafaka kwa wanawake
kujiendeleza na kujiimarisha.’’
Rais wa Mauritania Muhammed Walad Abdulaziz
aliyekuwa rais wa AU wa awamu iliyopita,
alimwachia kiti Rais wa Zimbabwe Robert
Mugabe tarehe 30 Januari.
Robert Mugabe aliyezaliwa mwaka wa 1924 ,
akawa Waziri Mkuu mwaka wa 1980 na kisha
kukalia kiti cha urais mwaka wa 1987 , amekuwa
ni rais mwenye umri mkubwa zaidi duniani
aliyekuwa madarakani.
Chanzo:bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top