Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) ametoa
shutuma zake bungeni Dodoma akimtuhumu
mbunge James Mbatia kuwa amekuwa
akimpakazia mambo mabaya kwa wapiga kura wa
jimbo lake kuwa ana UKIMWI. Mrema amesema
kuwa mbunge huyo amekuwa akipita jimboni
kwake na kusema kuwa wasimchague mbunge
huyo kwa kuwa ana UKIMWI na hana maisha
marefu hapa duniani. Ametoa kauli hiyo bungeni
Dodoma na kusema "Napenda kusema kuwa mimi
ni mbunge halali wa Vunjo na Mbatia hatapata
jimbo hilo, na natangaza kuwa nitagombea tena na
hafi mtu hapa"
MJUMBE BLOG
Tunashukuru kwa kututembelea.
Post a Comment